Loading...

Makambo aletewa kiatu maalumu toka Uturuki


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo hivi karibuni anatarajia kupokea kiatu kipya cha kuchezea kutoka nchini Uturuki baada ya kununuliwa na mmoja wa wafuatilia wa soka nchini Tanzania, Mzee Karama.

Mdau huyo mwenye duka la mich­ezo la Just Fit lililopo Mlimani City jijini Dar amemnunulia kiatu hicho mshambuliaji huyo sambamba na beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambavyo atawapa hivi karibuni kwa ajili ya kuvi­tumia kwenye michezo ya ligi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Champion, Mzee Karama amesema kuwa anamletea Makambo viatu hivyo kwa ajili ya kuongeza idadi ya mabao ambapo tayari ameshavilipia.

“Nipo Uturuki na nimenunua viatu vya Makambo na Ninja ambavyo nawaletea, tayari nime­shavilipia. Namletea Mkambo hili ma­bao yaongezeke,” alisema Mzee Karama.
Makambo aletewa kiatu maalumu toka Uturuki Makambo aletewa kiatu maalumu toka Uturuki Reviewed by Zero Degree on 12/21/2018 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.