Loading...

Simba yaichakaza Nkana FC bao 3-1 Taifa


Mechi ya marudiano ya hatua ya kwanza kuwania kufunzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Nkana FC ya Zambia imemalizika kwa Simba kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Dakika 5 za mwanzo Simba walianza vizuri ila ndani ya dakika 15 walipoteana na kuruhusu bao la dakika ya 16 lililofungwa na Walter Bwalya baada ya kushambulia lango la Simba kwa muda mrefu.

Iliwalazimu Simba wasubiri mpaka dakika ya 29 akimalizia pasi ya Claytous Chama na dakika ya 45 Meddie Kagere aliandika bao kwa kichwa akimalizia pasi ya James Kotei.

Kipindi cha pili dakika ya 88 Claytous Chama alifunga bao akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.

Simba wanafanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3.
Simba yaichakaza Nkana FC bao 3-1 Taifa Simba yaichakaza Nkana FC bao 3-1 Taifa Reviewed by Zero Degree on 12/23/2018 06:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.