UEFA: Liverpool, Tottenham zatinga 16 bora
Liverpool wamefuzu kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Napoli.
Klabu hiyo ya Anfield ilihitaji ushindi bila kufungwa au ushindi wa mabao mawili ya wazi ndipo kufika hatua ya 16 bora.
Salah alitekeleza wajibu wao kwa kumbwaga kipa David Ospina aliyekuwa analinda lango la Napoli dakika ya 34. Salah alikuwa amefunga mabao matatu katika ushindi wa Liverpool wa 4-0 wikendi Ligi ya Premia dhidi ya Bournemouth.

Ospina alifidia kwa kuwazuia Salah na Sadio Mane kufunga baadaye kwenye mechi hiyo, Virgil van Dijk naye akakosa nafasi ya wazi ya uongeza ushindi wa Liverpool.
Kutokufungwa kwa Liverpool zaidi kulichangiwa na kipa wao Alisson aliyekomboa shuti kali kutoka kwa Arkadiusz Milik katika shambulio nadra la Napoli kwenye mechi hiyo iliyochezewa Anfield.
Kipa huyo Mbrazil alijiunga na klabu hiyo ya Uingereza kutoka AS Roma mwezi Julai kwa uhamisho uliovunja rekodi kwa magolikipa, ambapo alilipiwa £66.8m.

"Ningelijua kwamba Alisson alikuwa mzuri hivi, ningelipa bei yake maradufu," alisema Klopp baada ya mechi hiyo.
"Na bao hilo la Mo - bao zuri ajabu - lakini kwa Ali (Allison) sina cha kusema kwa sasa. Alikuwa mkombozi."
Liverpool wamesonga kwa kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Paris St-Germain -mafanikio ambayo wameyapata licha ya kushindwa mechi tatu za ugenini katika kundi lao.Image captionAlisson alimzuia Milik kufunga
Klabu hiyo ya Uingereza ambayo ilishindwa na Real Madrid kwenye fainali msimu uliopita, itakutana na mshindi wa mojawapo ya makundi katka hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya droo itakapofanywa 17 Desemba.

Walishindwa 3-1 mjini Kiev katika mechi ambayo kipa wao Loris Karius alifanya makosa kadha naye Mo Salah akaumia.
Droo hiyo huenda ikawakutanisha na Real Madrid, au Barcelona, klabu ya zamani ya Klopp Borussia Dortmund na Porto ya Ureno, klabu ambazo tayari zimefuzu zikiwa zinaongoza katika makundi yao.
Matokeo ya mechi za UEFA Jumanne Tarehe 11 Desemba, 2018
- Schalke 1-0 Lokomotiv Moscow
- Galatasaray 2-3 FC Porto
- Club Brugge 0-0 Atletico Madrid
- Monaco0-2 Borussia Dortmund
- Barcelona 1-1 Tottenham
- Inter Milan 1-1 PSV Eindhoven
- Red Star Belgrade 1-4 Paris Saint Germain
- Liverpool 1-0 Napoli
Tottenham walitimiza kilichodhaniwa na wengi kwamba hakiwezekani, kwa kufuzu kwa hatua ya 16 bora, kwa mujibu wa meneja wao Mauricio Pochettino.
Lucas Moura alifunga bao la dakika 85 na kusawazisha dhidi ya Barcelona uwanjani Camp Nou na kuwapa alama muhimu Kundi B, baada yao kuzoa alama moja pekee kutoka kwa mechi zao tatu za kwanza.

Walikuwa wanahitaji kufikia matokeo ya Inter Milan dhidi ya PSV Eindhoven au wapate matokeo bora zaidi ya hayo. Waliondoka na ushindi wa 1-0.
Walikuwa hatarini kuondolewa baada ya Mauro Icardi kusawazisha bao la mapema la PSV nao Barca wakawa wanaongoza kwa kipindi kirefu mechi hiyo kupitia bao la Ousmane Dembele la dakika ya saba.
Lakini Moura aliwaokoa, na baadaye wakawa wanasubiri kusikia iwapo Inter walikuwa wamefunga bao la ushindi, ambalo kwa bahati yao halikutokea.Image captionDembele (pili kulia) amekosolewa sana kutokana na vituko vyake nje ya uwanja lakini sasa amefunga mabao tisa katika mechi 25
"Nina furaha sana kwa sababu ya mashabiki - huu ni ufanisi mkubwa sana, mkubwa ajabu kwa klabu hii," alisema Pochettino.

Reviewed by Zero Degree
on
12/12/2018 07:20:00 AM
Rating: