Loading...

Waziri wa ulinzi wa Marekani amejiuzulu

Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis ataondoka rasmi kazini mwezi Februari mwakani


Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis, amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa utawala wa Bwana Donald Trump.

Bwana Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter, akisema kuwa Jenerali huyo atastaafu "Kwa heshima na taadhima" mwishoni mwa mwezi Februari mwaka ujao.

Hilo linatukia siku moja tu baada ya tangazo la Rais lililosababisha utata mkubwa, kwamba Marekani imeamua kuyaondoa majeshi yake kutoka Syria.

Kwenye barua yake, Jenerali Mattis, kwa uzito mkubwa, aligusia kiini cha kujiuzulu kwake kwamba kumesababishwa na tofaurti za sera aliyo nayo na ile ya Bw Trump.

Idadi kubwa ya wanachama wakuu wa chama chake Trump cha Republican, wamelichukulia swala hilo kujiuzulu kwa Jenerali Mattis kwa uzito mkubwa.

Kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Seneti, Mitch McConnell amesema kwamba, "ana huzuni kubwa" kwa kuondoka kwa Mattis kwa sababu ya "kutofautiana" kati ya Jenerali Mattis na Rais.

Bwana Trump hajamtaja mtu kuchukua mahala pake, lakini amesema atafanya hivyo muda mfupi ujao.

Kuondoka kwa waziri huyo wa ulinzi ni hatua ya hivi punde zaidi katika msururu wa viongozi wakuu katika utawala wa Trump kujiuzulu au kufutwa kazi, tangu Trump alipochukua hatamu za uongozi.

Chanzo: BBC
Waziri wa ulinzi wa Marekani amejiuzulu Waziri wa ulinzi wa Marekani amejiuzulu Reviewed by Zero Degree on 12/21/2018 03:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.