Loading...

Manchester City hoi, United yanusurika kichapo Ligi Kuu ya Uingereza


Matumaini ya Manchester City kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi ya Premia (EPL) kwa msimu huu yamekumbana na gharika baada ya kukubali kichapo cha goli mbili mbele ya Newcastle Jumanne usiku. Kwa upande wa Manchester United chupuchupu wakubali kipigo dhidi ya Burnley baada ya magoli mawili ya kusawazisha dakika za lala salama.


City walisafiri hadi ugenini katika uga wa St James’ Park, na waliuanza mchezo kwa kasi na kupata goli la utangulizi katika sekunde ya 24 ya mchezo kupitia mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Aguero.

Hata hivyo ulegevu katika safu ya ulinzi ya City ulimpa mwanya Salomon Rondon katika dakika ya 66 kufunga goli maridhawa akiunganisha pasi ya kichwa kutoka kwa Isaac Hayden.

Mchezo huo ulibadili muelekeo katika dakika ya 78 baada ya Newcastle ama maarufu kwa jina la Magpies walipata penati baada ya kiungo wa City Fernandinho – kumfanyia madhambi Sean Longstaff kwenye eneo la hatari.

Matt Ritchie alisubiri kwa takriban dakika mbili kabla ya kupiga mkwaju wa penati wakati kipa wa City Ederson akipokea matibabu.

Mchezo huo ulibadili muelekeo katika dakia ya 78 baada ya Newcastle ama maarufu kwa jina la Magpies walipata penati baada ya kiungo wa City Fernandinho – kumfanyia madhambi Sean Longstaff kwenye eneo la hatari.

Matt Ritchie alisubiri kwa takriban dakika mbili kabla ya kupiga mkwaju wa penati wakati kipa wa City Ederson akipokea matibabu.

Mkwaju huo ulipigwa katika dakika ya 80 na ulipeleka kilio kwa mashabiki wa City.

Manchester United chini ya kucha wao wa muda Ole Gunnar Solskjaer nusura wakumbane na kichapo chao cha kwanza baada ya kushinda mechi nane toka kocha huyo achukue uongozi wa timu.

United walitanguliwa na Burnley kwa goli mbili sifuri na kusawazisha katika dakika za lala salama na kuambulia lama moja.

Magoli ya Burnley yalifungwa na Ashley Barnes katika dakika ya 51 na Chris Wood katika dakika ya 81.

Pogba alisawazisha goli la kwanza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 87 na dakika ya 92 Victor Lindelof aliihakikishia sare United.
Manchester City hoi, United yanusurika kichapo Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City hoi, United yanusurika kichapo Ligi Kuu ya Uingereza Reviewed by Zero Degree on 1/30/2019 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.