Mbunge Chadema amkumbuka JK
Meiseyeki amelitaja jina la kiongozi huyo Mstaafu Kikwete wakati akiuliza swali kwenda kwa Wizara ya ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) juu ya ujenzi wa barabara ambayo aliahidi Rais Jakaya Kikwete kipindi cha utawala wake ambayo mpaka sasa bado haijajengwa.
"Mheshimiwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliahidi ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 12 lakini mpaka sasa bado serikali haijatekeleza ahadi hiyo." ameuliza Mbunge Meiseyeki
Akijibu swali hilo Naibu Waziri TAMISEMI Joseph Kakunda amesema,"ni kweli Rais Kikwete aliahidi wa ujenzi wa barabara hiyo mwezi Novemba 2012 lakini serikali ilishaanza utekelezaji wa ahadi hiyo ya Jakata Kikwete mwaka 2014/2015 barabara zenye urefu wa kilomita 3.5 zimeshajengwa".
Chanzo: Eatv
Mbunge Chadema amkumbuka JK
Reviewed by Zero Degree
on
1/29/2019 08:05:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
1/29/2019 08:05:00 AM
Rating:
