Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Januari 30, 2019
Real Madrid wanampango wa kumsajili straika wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic, 21 - ambaye yupo kwa mkopo kutoka Benfica - ili awa mrithi wa wa streka raia wa Ufaransa Karim Benzema. (AS)
Arsenal na Manchester City wamejiunga katika mbio za usajili wa kiungo wa Everton na timu ya taifa ya Senegal, Idrissa Gueye, 29.
Kinda wa Benfica Mesaque Dju, 19, anatarajiwa kujiunga na West Ham kama mchezaji huru. (Sky Sports)
Hata hivyo Everton wanasubiri ofa kutoka klabu ya Paris St-Germain kwa ajili ya Gueye. (Daily Mail)
Southampton wamo mazungumzoni na Olympiakos ili wamsajili beki raia wa Norway Omar Elabdellaoui, 27. (Sun)
Arsenal, West Ham na Newcastle wote wametangaza dau kutaka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Monaco Mbelgiji Youri Tielemans 21. (Star)
Kaka wa nyota Paul Pogba, Florentin, 28, ianatarajiwa kujiunga na klabu ya Atlanta United inayocheza ligi ya soka ya Marekani MLS inayonolewa na Mholanzi Frank de Boer. (L'Equipe)
![]() |
Abdulkadir Omur |
Liverpool wanahusishwa na usajili wa kiungo kinda wa klabu ya Trabzonspor Abdulkadir Omur, 19, ambaye anawaniwa na klabu kadhaa barani Ulaya kwa sasa. (iNews)
Kocha Rafael Benitez kwa mara ya kwanza ameweka wazi kuwa hana hakika kama ataendelea kuiinoa klabu ya Newcastle United baada ya msimu kumalizika. (Independent)
Newcastle wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo kiungo Andreas Samaris, 29, kutoka Benfica. (Chronicle)
Newcastle wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo kiungo Andreas Samaris, 29, kutoka Benfica. (Chronicle)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Januari 30, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
1/30/2019 10:50:00 AM
Rating:
