Loading...

Wawili wafariki dunia baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto



WATU wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya magari mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na kisha kuwaka moto na kuteketea kabisa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Willbroad Mutafungwa alithibitisha jana ajali hiyo ilitokea eneo la Makunganya katika Manispaa ya Morogoro kwenye Barabara Kuu ya Morogoro – Dodoma. Kamanda Mutafungwa alisema ajali hiyo ilitokea saa 11 alfajiri ikihusisha gari lenye namba za usajili T.661 DKS aina ya Leyland Ashok ambalo ni la kuchimba visima lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma lililogongana na lori aina ya MAN lenye namba za usajili JA. 4417/ T.0806 likitokea Dodoma.

Alisema lori Man lilibeba mkaa na kuwaka moto na kutekeza magari yote na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine wawili waliopelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kutibiwa. Alisema Polisi walifika eneo la ajali na juhudi za kuzima moto huo zilichukuliwa ingawa magari hayo yaliteketea lakini waliyaondoa barabarani baada ya kuziba njia na kuwezesha magari mengine kupita.

Alisema baada ya kuudhibiti moto huo na kuchunguza ndani ya magari hayo, walikuta watu wawili wameshafariki dunia ambao aliwataja kuwa ni Mzambile Sadoki (27) ambaye ni dereva wa gari aina ya Man, raia na mkazi wa wa Burundi aliyekuwa akitokea nchini humo kwenda jijini Dar es Salaam. Mwingine ni dereva wa Leyland Ashok, Chekeli Redy (45) mkazi wa Morogoro aliyekuwa akitokea Dodoma. Aliwataja majeruhi kuwa ni Mateso Hassan (32) mkazi wa Morogoro aliyekuwa kwenye gari kutoka Burundi, Madua Zuberi (25) mkazi wa Burundi aliyekuwa kwenye gari la kwenda Dodoma. Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, uchunguzi wa Polisi unafanyika ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Wawili wafariki dunia baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto Wawili wafariki dunia baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto Reviewed by Zero Degree on 1/30/2019 12:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.