Loading...

Bado ninaweza kucheza soka katika Ligi Kuu ya Uingereza - Rooney


Wayne Rooney amesema kwamba bado ana uwezo wa kucheza soka katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Nyota huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza Wayne Rooney amesema kwamba bado ana uwezo wa kucheza soka katika Ligi Kuu ya Uingereza, EPL. Kwa sasa nyota huyo wa zamani wa Everton na Manchester United anakipiga katika klabu ya DC United nchini Marekani baada ya kuondoka Everton mwishoni mwa msimu uliopita.

Mbali na kuwa kinara wa mabao Uingereza, straika huyo mwenye umri wa miaka 33 pia aliandika rekodi nzuri ya mabao katika miaka yake 10 akiwa Manchester United.

Akizungumza na CNN, nyota huyo alisema, “Kusema kweli, naujua ubora wangu vizuri, bado nina uwezo wa kucheza katika Ligi Kuu ya Uingereza.”

Alisema, “Nalitambua hilo. Siku zote nimekuwa mtu anayejiamini, na hivyo nina matarajio mengi. Ndio, nimekuja hapa nikiwa namatarajio ya kufanya vyema. Na ninafikiri kwamba kulikuwa na mshituko kidogo kwa watu wambao walikuwa na maoni yao, ambapo ni hakaki, lakini kamwe sijawahi kujishuku uwezo wangu.”

Akimzungumzia kaimu meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, Rooney alisema, “Ole Gunnar ni mtu safi sana. Nafikiri, klabu itabidi ifanye uamuzi sahihi mwishoni mwa msimu, na ingekuwa vizuri kuona Ole akiendelea na kasi hii, na kupewa mkataba wa kudumu. Lakini kama si yeye, kama klabu itaamua kutafuta mbadala kutoka sehemu nyingine, basi nafikiri kwa mtazamo wangu Pochettino angekuwa mtu sahihi.”
Bado ninaweza kucheza soka katika Ligi Kuu ya Uingereza - Rooney Bado ninaweza kucheza soka katika Ligi Kuu ya Uingereza - Rooney Reviewed by Zero Degree on 2/06/2019 01:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.