Loading...

Tunapenda kutangaza msiba kuliko uponyaji - Makonda


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewajia juu baadhi ya watu ambao wameonesha kutuunga mkono wimbo wa msanii, Ommy Dimpoz ambao unajulikana kwa jina la 'Ni wewe' uliolenga kutoa shukrani kwa Mungu.

Kupitia ukurasa wake instagram, Makonda amesema amechukizwa na kile alichokiita ni unafki kwa baadhi ya watu ambao mwanzoni wakati anaumwa walioneshwa kuguswa na uhai wake lakini baada ya kutoa wimbo hakuna hata mmoja anayeunga mkono.

Makonda ameandika, "ukitaka kujua watu walivyo wa ajabu tazama leo, Ommy Dimpoz alikuwa mgonjwa sana na ikafika hatua ya watu kutangaza amekufa, leo amerejea tena akiwa na wimbo wa kumshukuru Mungu wamekaa kimya kama vile siyo wao waliokuwa wana post kumwombea apone".

Aidha Makonda ameendelea kuandika, "angefariki tungeona mitandao yote imechafuka RIP Ommy oooh umeenda bado tunakuhitaji, unafiki huu sijui utaisha lini, tunapenda kutangaza msiba kuliko uponyaji".

Msanii huyo amerejea nchini mapema wiki hii alipokuwa akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.
Tunapenda kutangaza msiba kuliko uponyaji - Makonda Tunapenda kutangaza msiba kuliko uponyaji - Makonda Reviewed by Zero Degree on 2/06/2019 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.