Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Februari 6, 2019


Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 28,anatarajiwa kuiambia klabu hiyo kuelekea Real Madrid mwisho wa msimu huu. (Telegraph)

Real Madrid wana matumaini ya kumsaini raia huyo wa Ubelgiji na wako tayari kutumia £100m kukamilisha makubaliano hayo. 

Tottenham ina mipango ya kuimarisha hamu yao ya kumsajili kinda wa Norwich Max Aarons kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu. (Mirror)
Eric Bailey ,24, ameambiwa na kaimu mkufunzi Ole Gunnar Solskjiaer kwamba anasalia kuwa miongoni mwa mipango yake katika klabu ya Old Trafford.

Lakini beki wa kati wa United Eric Bailey ,24, ameambiwa na kaimu mkufunzi Ole Gunnar Solskjiaer kwamba anasalia kuwa miongoni mwa mipango yake katika klabu ya Old Trafford.

Kuondoka kwa Hazard kunaweza kusababisha mikataba ya uhamisho, ikiwemo ile ya kiungo wa kati wa Real Madrid Mateo Kovacic, 24, ambaye uhamisho wake wa, mkopo katika klabu hiyo ya Stamford bridge utafanywa wa kudumu pamoja na ule wa kinda wa Uingereza winger Callum Hudson-Odoi, 18, ambaye anauzwa katika klabu ya Bayern Munich. (Sun)

Chelsea huenda hivi karibuni pia ikampoteza mshambuliaji Willian 30 kwa sababu wanataka kumuongezea kandarasi ya mwaka mmoja raia huyo wa Brazil wakati kandarasi yake itakapokamilika katika kipindi cha miezi 18 , badala ya makubaliano ya muda mrefu.

Kalidou Koulibaly

Lengo la Man United katika dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu ni beki wa kati huku beki wa Napoli Kalidou Koulibaly , 27 akiwa chaguo la miamba hiyo ya Manchester. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko,24, ana hamu ya kutaka uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya AC Milan kuwa wa kudumu.

Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko ana hamu ya uhamisho wa mkopo katika klabu ya AC Milan kuwa wa kudumu. (Football London)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Februari 6, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatano Februari 6, 2019 Reviewed by Zero Degree on 2/06/2019 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.