Hatimaye Kichuya atimkia Misri
Kwa mujibu wa taarifa ya Eatv, Mtendaji mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema Kichuya amesaini mkataba wa miaka 4 na klabu hiyo pamoja na malipo mazuri ambayo hata Simba hawakuwa wanamlipa.
''Kichuya ni kijana wetu na klabu imefaidika naye sana hivyo tunafurahi amepata timu ya daraja la pili na itamlipa vizuri na sisi kama Simba tumepata maslahi mazuri kwahiyo tumemuuza'', amesema.
Kichuya ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar atacheza ligi kuu ya Misri licha ya kuwa amesajiliwa na Pharco ambapo kwa mujibu wa Magori ni kwamba tayari timu hiyo imemtoa kwa mkopo katika klabu ya Enppi inayoshiriki ligi kuu.
Tayari Kichuya amesharipoti katika timu ya Enppi na kesho Februari 1, 2019 ataanza mazoezi na timu yake ya Enppi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Jumanne Februari 5, 2019.
Enppi inashika nafasi ya 14 kati ya 18 zinazoshiriki ligi kuu. Timu hiyo imecheza mechi 20, imeshinda 4, sare 9 na kufungwa mechi 7.

Reviewed by Zero Degree
on
2/01/2019 06:20:00 AM
Rating: