Antony Martial asaini mkataba mpya Manchester United
Martial mwenye miaka 23, alijiunga na United kutoka Monaco Septemba 2015 kwa pauni milioni 36, lakini hakuwa na furaha klabuni hapo mwaka 2018 na kocha aliyepita Jose Mourinho alikuwa radhi kumuuza.
Mkataba wake mpya utamfanya asalie na Mashetani Wekundu mpaka atakapotimu miaka 29, na kuna kipengele kinachoruhusu mkataba huo kuongezwa kwa mwaka mmoja.
Mkataba wake mpya utamfanya asalie na Mashetani Wekundu mpaka atakapotimu miaka 29, na kuna kipengele kinachoruhusu mkataba huo kuongezwa kwa mwaka mmoja.
Kocha wa muda wa United Ole Gunnar Solskjaer amesema: "Kwa umri wake, ana ubongo mzuri wa mpira, ambao, ukijumuishwa na kipaji chake cha kipekee kinamfanya awe mchezaji mwenye mustakabali mzuri kabisa."
Mwezi Juni, ajenti wa Martial alisema mteja wake alikuwa anataka kuhama, na Mourinho alikwa radhi, lakini uongozi wa United ulizima jaribio hilo na wakafungua ukurasa mpya wa majadiliano.
"Ningependa kumshukuru Ole na benchi lake la ufundi kwa kuniamini na kunifanya nikue mchezoni. Nafurahia wakati wangu klabuni. Toka siku nilipojiunga nimekuwa sehemu ya familia ya United na mapenzi ya mashabiki yamekuwa nguzo yangu," amesema Matial.
Antony Martial asaini mkataba mpya Manchester United
Reviewed by Zero Degree
on
2/01/2019 06:05:00 AM
Rating: