Loading...

Burnley kumrejesha Peter Crouch EPL



Kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, Peter Crouch atasaini mkataba na klabu ya Burnley siku ya kufungwa kwa dirisha la usajili wakatu Sam Vokes akielekea Stoke City.

Vokes alijiunga na Burnley akitokea Wolves mwaka 2012 anawe akaondoka kujiunga na klabu hiyo inyaoshiriki Championship mwisho wa siku kwa kubadilishana na Crouch pamoja na kipengele cha kuweza kumnunua tena kwa kiasi cha pauni milioni 9.

Sean Dyche alisita kumwachia mshambuliaji wake huyo mwenye magoli 6 aondoke katikati ya msimu bila kusajili mbadala wake. Makubaliano yamefikiwa ambapo, Crouch atashuhudiwa akirejea Ligi Kuu ya Uingereza siku moja baada ya kusherehekea kufikisha umri wa miaka 38.

Nyota huyo wa zamani wa Uingereza ana magoli 106 EPL, akiwa amechezea vilabu kama Liverpool, Tottenham Hotspur, Southampton na Portsmouth. Kwa bahati mbaya amefanikiwa kufunga goli moja tu katika michezo 23 tangu ajiunge na Stoke msimu huu.

Crouch anaweza kuwa kwenye nyakati za mwisho za maisha yake ya soka lakini urefu wake ukijumlisha na uzoefu wake bado vinampa sifa ya kuwa mshambuliaji tishio awapo uwanjani.
Burnley kumrejesha Peter Crouch EPL Burnley kumrejesha Peter Crouch EPL Reviewed by Zero Degree on 1/31/2019 02:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.