Mashabiki wajiandae kusikiliza kazi yetu mpya - Weusi
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, John Makini ‘Joh Makini’, alisema walipanga kuingiza kazi mpya sokoni mapema wiki iliyopita.
Alisema sababu iliyowakwamisha ni msiba wa msanii Godzilla, hivyo tayari muda wowote kuanzia sasa wataachia kazi mpya.
“Tulipisha msiba wa msanii mwenzetu Godzilla, mashabiki wajiandae kusilikia kazi yetu mpya tuliyoshirikiana na wasanii kutoka nchini Kenya,” alisema Joh Makini.
Joh Makini alisema wimbo wao umepewa jina la ‘Kutulia’, huku wakiwa wamewashirikisha Sautisol.
Mashabiki wajiandae kusikiliza kazi yetu mpya - Weusi
Reviewed by Zero Degree
on
2/23/2019 03:15:00 PM
Rating: