Mbunge ataka wabunge ambao hawajatahiriwa wakaguliwe
Mbunge maalum Jackline Ngonyani amependekeza hatua hiyo katika hoja ya kujadili udhibiti wa maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini.
Akizungumza bungeni, Mbunge huyo ameeleza bunge kwamba lengo la 90-90-90 la virusi vya ukimwi litafikiwa nchini Tanzania, pale kutakuwa na ridhaa ya watu kujipima wenyewe.

Ameeleza kwamba changamoto kubwa ni kutokana na kuwa baadhi ya watu wanoana aibu kupimwa vituoni, hasaa wanaume.
Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na VVU/AIDS (UNAIDS) na washirika wake, walizindua lengo la 90-90-90 ambalo limenuia; kutambua kwa 90% watu wote walioathirika na virusi vya Ukimwi, kutoa matibabu ya dawa za kuzuia makali ya VVU kwa 90% ya waliotambuliwa, na kufanikiwa kudidimiza kusambaa kwa virusi kwa 90% kwa waliotibiwa kufikia 2020.
'Suala la mkono sweta, ni tatizo kubwa, ili kufikia 90-90-90 ni lazima tuhakikishe kwamba mikono sweta yote imeondolewa' amesema mbunge Jackline Ngonyani.
Bi Ngonyani amependekeza, 'Nashauri tuanze na wabunge humu ndani ambao watabainika hawajafanya hiyo tohara ili wafanyiwe tohara mara moja'.
Mbunge huyo amesisitiza kwamba wengi wanaona aibu kwenda kupima, lakini iwapo kutakuwa na utaratibu unaofuatwa wa kila mmoja kujipima mwenyewe itakuwa ni vyema na kusaidia kupunguza kusambaa kwa virusi vya ukimwi nchini.

Utafiti uliofanywa kwa wingi kweli, umebaini kwamba wanaume ambao hawajatahiriwa wana nafasi ya kuambukizwa na kuenezea maambukizi mbali mbali ikiwemo ya ugonjwa wa ukimwi.
Shirika la afya duniani WHO linasema kupasha tohara kunapunguza hatari ya wanaume kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60.
Wabunge waliopashwa tohara Africa kupunguza HIV
Wabunge karibu 10 nchini Zimbabwe walitahiriwa katika operesheni iliyoidhinishwa nchini mnamo 2012 katika kukabiliana na kusambaa kwa virisi vya Ukimwi nchini humo
Nje ya majengo ya bunge mjini Harare , kulijengwa zahanati ndogo kwa sababu ya shughuli hizo za kuwapasha wabunge tohara.
Nia ilikuwa ni kuchochea wanaume nchini Zimbabwe kutahiriwa kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Wabunge hao walijitokeza hadharani ili kupimwa hali yao ya Ukimwi.
Zimbabwe ni moja wapo wa mataifa 13 barani Afrika ambapo mwaka 2007, shirika la WHO lilisema kuna haja kubwa ya kuanzisha harakati za kuwatahiri wanaume.

Chanzo: BBC
Mbunge ataka wabunge ambao hawajatahiriwa wakaguliwe
Reviewed by Zero Degree
on
2/08/2019 07:20:00 AM
Rating: