Simba walisahau kwamba Al Ahly ni timu bora - Cannavaro
Cannavaro ambaye kwa sasa ni meneja wa Yanga, ameyasema hayo kufuatia Simba kupoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri kwa kipigo cha mabao 5-0, wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Borg EL Arabi nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Cannavaro alisema sababu kubwa Simba kupokea kipigo hicho kizito ni kutokana na kushindwa kucheza kwa malengo huku beki yao ikionekana kuwa nyepesi kupitika.
“Kilichotokea kwa Simba ni kama walikitaka wenyewe kwa sababu kwanza hawakutaka kuwaheshimu wapinzani wao lakini walisahau kwamba Al Ahly ni bora maana ukiangalia walicheza bila ya kuwa na malengo yoyote ndiyo maana wakapokea kipigo.
“Unapocheza na timu bora kwanza lazima uwe na mpango wa kwanza na wa pili lakini Simba hawakuwa nayo, pia walikosa wachezaji wa kuamua matokeo na kujitolea maana hata ukiangalia beki yao ilikuwa nyepesi kupitika na kuruhusu bao tano kwenye kipindi cha kwanza. Nafasi bado wanayo iwapo wakijipanga vizuri,” alisema Cannavaro.
Simba walisahau kwamba Al Ahly ni timu bora - Cannavaro
Reviewed by Zero Degree
on
2/08/2019 07:15:00 AM
Rating: