Loading...

Watumishi 9 wizara ya ardhi wafariki ajalini


Watumishi tisa kati ya 13 wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wamefariki dunia katika ajali ya gari.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Februari 23, 2019 saa 11 jioni baada ya gari hiyo mali ya Serikali STK 9444 kutumbukia mto kikowila uliopo katikati ya Kiberege na Mji wa Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro.

Watumishi hao 13 waliokuwa kwenye gari hiyo aina ya Land Cruiser walikuwa wakitoka kwenye shughuli za upimaji ardhi zinazoendelea wilayani humo.

Manusura wa ajali hiyo wamelazwa hospitali ya St. Francis mkoani Morogoro kwa matibabu

Kwa mujibu wa taaifa ya Mwananchi, Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo amethibitidha kutokea kwa ajali hiyo, sasa kinachofanyika ni kuwataarifu ndugu wa marehemu na taratibu nyingine zinaendelea.

Amesema kamati ya ulinzi na usalama itakutana kesho Jumapili asubuhi kwa ajili ya taarifa zaidi.

Endelea kufatilia blog yetu kwa habari zaidi juu ya ajali hii.








Watumishi 9 wizara ya ardhi wafariki ajalini Watumishi 9 wizara ya ardhi wafariki ajalini Reviewed by Zero Degree on 2/24/2019 07:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.