IGP Sirro atangaza neema kwa madereva
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, alitoa wito huo jana, alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu changamoto za faini wanazotozwa madereva wa magari katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema madereva wanaohisi wameonewa na askari hao wasikubali kulipa faini na ikiwezekana wakubali kwenda mahakamani kama wakishindwa kuwasilisha malalamiko yao ngazi za juu kwa sababu jeshi hilo halina lengo la kuwaonea wananchi wake.
"Inapotokea dereva anahisi ameonewa asikubali kulipa faini, asilipe fedha yoyote, awasiliane na viongozi na aende kwa Mkuu wa Usalama Barabarani amuelezee tatizo lake na ikishindika akubali kwenda mahakamani badala ya kulipa faini ya kuonewa," alisema Sirro.
Alisisitiza kuwa, askari hao hawapaswi kumuonea mtu yeyote na inapotokea hivyo madereva wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi.
"Kiongozi kama umefuatwa kuna malalamiko umepewa unapaswa uchukue hatua za haraka kwa sababu viongozi wa juu wanapaswa kusimamia vyema majukumu yao," alisema IGP Sirro.
Alisisitiza kuwa, askari hao hawapaswi kumuonea mtu yeyote na inapotokea hivyo madereva wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi.
"Kiongozi kama umefuatwa kuna malalamiko umepewa unapaswa uchukue hatua za haraka kwa sababu viongozi wa juu wanapaswa kusimamia vyema majukumu yao," alisema IGP Sirro.
IGP Sirro atangaza neema kwa madereva
Reviewed by Zero Degree
on
3/02/2019 02:05:00 PM
Rating: