Juventus yaipa Chelsea mtihani mzito
Shinikizo hilo linatokana na ukweli kuwa Juventus inataka kumchukua Zidane kwa ajili ya msimu ujao wa soka.
Kuna taarifa kuwa kocha wa sasa wa Juventus, Massimiliano Allegri anatazamiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Allegri inasemekana anataka kuachana na timu hiyo baada ya kuisaidia kutwaa taji la Serie A kwa mara ya tano mfululizo.
Chelsea katika siku za karibuni inasemekana imekuwa inafanya mawasiliano na Zidane kwa ajili ya kumchukua.
Hali hiyo inatokana na mwenendo wa sasa wa kusuasua wa timu hiyo inayonolewa na Maurizio Sarri.
Hali hiyo inatokana na mwenendo wa sasa wa kusuasua wa timu hiyo inayonolewa na Maurizio Sarri.
Juventus, hata hivyo, inasemekanna inataka kumchukua Zidane, ambaye aliwahi kuchezea timu hiyo katika miaka ya nyuma.
Maana yake ni kuwa Chelsea inaweza kumkosa kama isipoongeza juhudi.
Hata presha ya kutimuliwa kwa Sarri imepoa kidogo baada ya kusaidia Chelsea kuishinda Tottenham Hotspur 2-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu England, Jumatano iliyopita.
Hata presha ya kutimuliwa kwa Sarri imepoa kidogo baada ya kusaidia Chelsea kuishinda Tottenham Hotspur 2-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu England, Jumatano iliyopita.
Juventus yaipa Chelsea mtihani mzito
Reviewed by Zero Degree
on
3/02/2019 01:50:00 PM
Rating: