Chadema yaweka wazi hatima ya Lissu urais 2020
![]() |
| Mwanasheria Mkuu wa chama cha Chadema, Tundu Lissu. |
Mashinji ameweka wazi kuwa chama kinaweza kumpa nafasi hiyo Lissu iwapo ataiomba.
Akizungumza na Nipashe kwenye mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Dk. Mashinji alibainisha kuwa Chadema huwapatia nafasi za kugombea wanachama wanaoomba, iwapo hapatakuwa na mwanachama yeyote aliyeomba ni jukumu la chama kutafuta mgombea miongoni mwa wanachama wake watakaonekana kuwa na sifa hiyo.
“Akiomba anaweza kupewa kwa sababu kwa mfumo wetu wa kugombea wanapewa nafasi watu walioomba na kama tutakosa mtu aliyeomba, basi tutatafuta mtu ambaye hajaomba,” alisema Dk. Mashinji.
Tetesi za Lissu kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka 2020 zilianza kuzagaa katika mitandao ya kijamii, ikimuhusisha kupitia muunganiko wa vyama vya ACT-Wazalendo na Chadema.
Vilevile, kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amekuwa akimtembelea mara kwa mara Lissu aliyeko Ubelgiji anakopatiwa matibabu kwa sasa.
Lakini wawili hao walipoulizwa na baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa, walieleza kuwa ukaribu wao kama wanasiasa wamekuwa wakikutana na kujadili masuala ya namna ya kujenga mapambano ya kujenga Tanzania mpya ya kidemokrasia na inayojadili haki za binadamu.

Dk. Mashinji akizungumzia zaidi kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini, alisema kupitia sekretarieti ya chama hicho, majina ya wote walioomba nafasi ya kugombea urais hufikishwa Kamati Kuu.
Alisema baada ya hapo Kamati Kuu hutoa idhini ya majina hayo kutangazwa, hivyo kutoa fursa ya kufanyiwa utafiti ili kupata jina moja litakalosimama kuwania urais.

MAANDALIZI YA ILANI
Kuhusu maandalizi ya ilani ya uchaguzi mkuu wa mwakani, Dk. Mashinji alisema chama hicho kimeshaanza mipango ya kukusanya taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau ili kutengeneza ilani itakayokuja na majibu ya masuala mbalimbali ya maendeleo.
“Ni jana tu tumemaliza kuweka taratibu za namna gani tutafanya hizo document (nyaraka), ni ilani inayolenga kukuza uchumi na kuiwezesha sekta binafsi kukua,” alisema Dk. Mashinji.

UCHAGUZI WA S/MITAA
Kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo upinzani umelalamikia kuwa kanuni zilizopo sio rafiki, Dk. Mashinji alisema kuwa pamoja na kuwapo kwa kanuni sizizo rafiki chama hicho hakina mpango wa kususia uchaguzi huo.
Alisema Chadema inatarajia kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka kwa wananchi.

Chanzo: Nipashe
Chadema yaweka wazi hatima ya Lissu urais 2020
Reviewed by Zero Degree
on
9/16/2019 08:50:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
9/16/2019 08:50:00 AM
Rating: