Loading...

Sadio Mane, Salah wamaliza tofauti zao


Sadio Mane amesema amemaliza tofauti zake na Mohamed Salah baada ya kutokea mzozo baina yake katika mechi dhidi ya Burnley.

Mshambuliaji huyo wa Senegal, alisema alikutana uso kwa uso na Salah na wamekubaliana kumaliza tofauti zao.

Mane aling’aka mbele ya Kocha Jurgen Klopp alipotolewa katika mchezo huo baada ya Salah kumtaka kurekebisha kasoro akiwa ndani ya eneo la hatari.

Mane hakufurahishwa na maelekezo ya nahodha huyo wa Misri na mara moja alimshambulia kwa maneno makali.

Kinara huyo wa mabao, alivua jezi na kuitupa chini alipokuwa katika benchi.

“Nini kuhusu Salah? Yamepita hayo,” alisema Mane baada ya kumalizika mchezo wa Ligi Kuu England walioshinda mabao 3-1 dhidi ya Newcastle United.
Sadio Mane, Salah wamaliza tofauti zao Sadio Mane, Salah wamaliza tofauti zao Reviewed by Zero Degree on 9/16/2019 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.