Loading...

Siwezi kuizungumzia Yanga kwa sasa - Kamusoko


KIUNGO wa Zesco United, Thabani Kamusoko, amesema sare waliyoipata ugenini dhidi ya Yanga kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, umempa matumaini ya timu yake kusonga mbele.

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Nipashe baada ya mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Taifa juzi na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, Kamusoko alisema anashukuru kuipatia bao la kusawazisha timu yake ugenini licha mchezo kuwa na presha pamoja na ushindani mkubwa.

"Nashukuru kwa bao ambalo nimelifunga ugenini, kwangu mimi ni faida kwa sababu kila timu ilikuwa inacheza kwa ushindani mkubwa ili ishinde," alisema Kamusoko.

Vile vile alisema lengo lake ni kujipanga akishirikiana na wachezaji wenzake kuhakikisha wanashinda na kutimiza malengo yao.

"Mikakati yangu kwa sasa ni kwenda kuanza maandalizi ya mchezo ujao nikishirikiana na wachezaji wenzangu ili tusonge mbele," alisema.

Alisema hawezi kuizungumzia Yanga kutokana na kuwa tayari alishaachana nayo na kudai kuna baadhi ya wachezaji ambao hawafahamu.

"Siwezi kuizungumzia Yanga kwa sababu sasa hivi nipo Zesco kuhusu ubora wa wachezaji pia siwezi kuuzungumzia kwa sababu sijawaona wakifanya mazoezi tumekutana uwanjani," alisema.

Mchezaji huyo aliyeifungia Zesco bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi, aliwahi kuitumikia Yanga kabla ya kuachwa na kutimkia Zambia kujiunga na 'Mafundi wa Umeme' hao.
Siwezi kuizungumzia Yanga kwa sasa - Kamusoko Siwezi kuizungumzia Yanga kwa sasa - Kamusoko Reviewed by Zero Degree on 9/16/2019 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.