Loading...

Suarez azungumzia kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Granada


MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Luis Suarez, amekiri mambo ni magumu ndani ya klabu hiyo baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Granada mchezo wa Ligi Kuu Hispania wikiendi iliyopita.

Katika mtanange huo ambao Barcelona walikuwa ugenini, Lionel Messi alianzia benchi baada ya kupona majeraha yaliokuwa yakimsumbua.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Suarez alisema huenda msimu huu mambo yakawa magumu kwao.

“Hatuwezi kuruhusu mabao kirahisi hivyo, ni dalili mbaya kwa upande wetu kupoteza nafasi nyingi za kufunga na hili limenipa hofu,” mshambuliaji huyo raia wa Uruguay.

Mabao ya Granada ambao wamepanda daraja msimu huu yaliwekwa kimiani na Ramon Azeez na Alvaro Vadillo kwa mkwaju wa penalti. Hii ni mechi ya nne mfululizo Barcelona haijashinda ugenini.
Suarez azungumzia kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Granada Suarez azungumzia kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Granada Reviewed by Zero Degree on 9/23/2019 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.