Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Septemba 23, 2019


Kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona Xavi, ambaye ni meneja wa timu ya Qatari ya Al-Sadd, anasema kuwa itakuwa ni tatizo kwake kuwaongoza wachezaji wenzake wa zamani kama vile Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets katika Nou Camp. (Ara)

Tottenham imetuma ujumbe kumchukunguza mchezaji wa kimataifa wa timu ya vijana waliochini ya miaka 21 wa Italia winga wa Fiorentina Riccardo Sottil ambaye ni mchezaji wa kiwango cha juu huku wakionyesha nia ya kumchukua kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 . (Express)

Romelu Lukaku anasema kuwa kocha wa klabu hiyo Antonio Conte ni mtu ambaye ''anamsaidia kila siku na humpa motisha''.

Matumaini ya klabu ya Chelsea ya kusaini mkataba na mchezaji wa Napoli Elseid Hysaj msimu ujao yanaweza kugonga mwamba huku klabu hiyo ya Italia ikiwa tayari kurefusha mkataba na kijana huyo kutoka Albania mwenye umri wa amiaka 25.

Meneja wa klabu ya Everton Marco Silva ameutuma ujumbe umchunguze zaidi straika wa RB Leipzig Yussuf Poulsen, mwenye umri wa miaka 25.(Express)

Roy Keane amesema kuwa "ameshtushwa na kusikitishwa " na namna klabu yake ya zamani ya Manchester United walivyoshindwa 2-0 na West Ham Jumapili. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 26, aliyejiunga na timu hiyo ya Italia kutoka Manchester United msimu huu, anasema kuwa kocha wa klabu hiyo Antonio Conte ni mtu ambaye ''anamsaidia kila siku na humpa motisha''. (Metro)

David de Gea


Meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho anasema golikipa wa Uhispania David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa na "bahati kidogo'' kupata mkataba mpya mzuri na klabu hiyo . (Sky Sports)

Mashabiki wapatao 1,000 wa Valencia waliandamana kabla ya mechi dhidi ya Leganes, kwa kutofurahishwa na namna mmiliki mwenza wa Salford City Peter Lim, na rais Anil Murthy anavyoendesha a klabu hiyo ya ligi ya La Liga. (Marca)

Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli, ambaye anaweza kuchezea Brescia dhidi ya Juventus Jumanne, anasema amefanya ''kazi kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopita "kuliko'' kipindi cha muongo mzima wa kazi yake'' huku kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 akilenga kupata nafasi katika kikosi cha nchi hiyo kitakachocheza kombe la Euro 2020. (Football Italia).

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Septemba 23, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Septemba 23, 2019 Reviewed by Zero Degree on 9/23/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.