Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Septemba 26, 2019
Uamuzi wa Ole Gunnar Solskjaer wa kutompa kiungo wa kati Paul Pogba fursa ya kuwa na nahodha wa Manchester United hauna uhusiano wowote na taarifa za kuhusishwa uhamisho wa Mfaransa huyo - ilikuwa ni kwasababu Axel Tuanzebe alikulia katika Rochdale.
Real Madrid inamtaka kiungo wa kati wa Tottenham raia wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, kusaini mkataba wa awali mwezi Januari - na baadae atahamia Spurs kwa meneja Mauricio Pochettino. (Mirror)
Mshambuliaji wa klabu ya RB Salzburg raia wa Norway Erling Braut Haaland, mwenye umri wa miaka 19, amedokeza kuwa atahamia katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kufunga mabao matatu katika gemu moja katika mchezo wa Championi Ligi.
Tottenham wanahofia Eriksen atakataa mapendekezo ya kumuuza mwezi Januari , hii ikimanisha kuwa anawza kuondoka kwa uhamisho usio na malipo msimu ujao.
Mshambuliaji wa timu ya Juventus Mario Mandzukic alikataa euro milioni 7 alizopewa kwa mwaka kuichezea timu ya Qatar kwa hiyo Mcroatia huyo mwenye umri wa miaka 33 ana fursa ya kujiunga na Manchester United mwezi Januari mwaka ujao.
Mchezaji mashuhuri wa Barcelona Xavi, ambaye kwa sasa ni kocha wa Qatar, anamuona mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 24, kama mchezaji anayefaa kusaini mkataba nae ikiwa wakati mmoja ataiongoza Nou Camp. (Mail)
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amejiandaa kumthamanisha mchezaji Harry Kane, mwenye umri wa miaka 26 katika kiwango cha thamani ya euro milioni 250 , kwa lengo la kuendelea kubaki na mshambuliaji huyo wa England hadi mwisho wa kile kinachoweza kuwa ni msimu mwingine Spurs kukosa kombe. (Telegraph)
Boca Juniors wametoa ofa yao ya kutaka kusaini mataba na mchezaji wa safu ya mashambulizi Mswiden Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 37, kutoka LA Galaxy. (AS)
Zlatan Ibrahimovic, 37 |
Meneja wa zamani ya klabu ya Manchester City amemuambia Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 28, kuwa anatakiwa kujiunga na Paris St-Germain ikiwa anataka kushinda Championi Ligi . (Het Nieuwsblad)
Makamu mwenyekiti mtendaji wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na Glazers kuhusu kufanya mabadiliko ya kile alichokitaja kama 'utamaduni ' katika klabu hiyo. (Express)
Barcelona wanataka kuhakikisha kwamba kiungo wa safu ya mashambulizi Ansu Fati mwenye umri wa miaka 16 hasafiri kuelekea katika michuano ya Kombe la dunia la vijana walio chini ya umri w amiaka 17 ili aweze kucheza gemu dhidi ya mahasimu wao Real Madrid tarehe 26 Oktoba. (Marca)
Manchester United walilazimika kumtafuta kiungo wa kati Peter Thomas kutoka Rochdale ambaye alikuwa mchezaji wa ziada na hatimae hakutumika kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Carabao Cup katika kipindi cha dakika 15 pekee. (Sun)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Septemba 26, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
9/26/2019 07:25:00 AM
Rating: