Utaratibu mpya kupata namba ya utambulisho wa taifa (NIN) watolewa
Taarifa iliyotolewa na Nida jana Jumatano Septemba 25, 2019 kupitia kitengo cha mawasiliano na hifadhi hati ilisema namba hiyo sasa imeanza kutolewa kupitia tovuti ya mamlaka hiyo kwa muombaji kutembelea https://services.nida.go.tz/nidpotal/get_nin.aspx.
Taarifa ya Nida ilibainisha kwamba huduma hiyo itawarahisishia waombaji wa vitambulisho vya Taifa kupata NIN bila kwenda ofisi za mamlaka hiyo.
Taarifa ya Nida ilibainisha kwamba huduma hiyo itawarahisishia waombaji wa vitambulisho vya Taifa kupata NIN bila kwenda ofisi za mamlaka hiyo.
Hatua za kufuta kupata namba ya NIN
- Tembelea tovuti ya NIDA ya www.nida.go.tz
- Bonyeza kitambulisho cha Taifa
- Fahamu namba ya utambulisho wa Taifa
- Andika jina lako la kwanza, jina la ukoo, tarehe ya kuzaliwa, jina la kwanza la mama na jina la mwisho la mama
- Bonyeza Tafuta
Aidha Nida imefafanua kuwa namba za NIN pia zimepelekwa ofisi za kata ili kuwapunguzia waombaji adha ya kufuata namba hizo ofisi za Nida za wilaya.
"Waombaji pia wanaweza kupata NIN kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenye kituo cha huduma kwa mteja," ilieleza taarifa hiyo.
"Waombaji pia wanaweza kupata NIN kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenye kituo cha huduma kwa mteja," ilieleza taarifa hiyo.
Utaratibu mpya kupata namba ya utambulisho wa taifa (NIN) watolewa
Reviewed by Zero Degree
on
9/26/2019 07:50:00 AM
Rating: