Loading...

Zimbabwe ya kwanza Afrika kuidhinisha sindano ya kuzuia Ukimwi (CAB-LA)



Harare: Zimbabwe imekuwa nchi ya kwanza Afrika na ya tatu duniani kuidhinisha matumizi ya dawa ya sindano ya kuzuia Ukimwi ya muda mrefu (CAB-LA) ambayo hivi karibuni imependekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) ndio ya kwanza kuidhinisha matumizi ya dawa hiyo nchini humo Desemba 2021 na Agosti 2022 Mamalaka ya Dawa na Bidhaa za Tiba ya Australia (TGA) ikatoa ridhaa ya matumizi ya dawa hizo.

Dawa ya CAB-LA hutolewa kwa njia ya sindano na hukinga maambukizi ya Ukimwi kwa muda mrefu, mtu huchomwa sindano mbili ambazo mhusika huwa kwenye uangalizi.

Ili kuwepo ufanisi wa dawa hiyo, WHO inasema, mtu hupaswa kutumia sindano kila baada ya miezi miwili.

Hatua ya Zimbabwe kuanza kutumia CAB-LA ni kufuatia vifo vinavyotokana na maambukizi ya Ukimwi nchini humo kuongezeka, ambapo 2002 inakadiriwa vifo 130,000 vilitokea hali ikiwa mbaya zaidi mwaka 2021 ambayo vilishuhudiwa vifo 20,000.

Mwaka jana Zimbabwe ilizindua mpango mkakati wa kudhibiti maambukizi ya Ukimwi kufikia 2030 unaofahamika kwa jina la 90-90-90.

Mpango huo una maana, asilimia 90 ya watu wenye maambukizi ya Ukimwi wawe wanajua hali zao, asilimia 90 ya wanaojua hali zao wawe wameanza dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi, asilimia 90 ya mwisho wanaotumia dawa wawe wamefubaza virusi hivyo.

Vituo vya afya nchini Zimbabwe vipo katika changamoto kubwa ya kutoa huduma bora za afya kutokana na uchumi mbovu, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa Zimbabwe (MCA) wiki iliyopita ilidhibitisha dawa hiyo kuidhinishwa nchini humo.

Taarifa ya WHO ambayo imethibitishwa na Mamlaka nchini Zimbabwe ilisema, ‘ni hatua muhimu’ ikiongeza itaisaidia Zimbabwe ‘kutengeneza na kuanzisha mipango’ ili CAB-LA itekelezwe kwa usalama na ufanisi ili iwe na matokeo makubwa.

Dawa hiyo imerejesha tumaini ya kupunguza vifo nchini Afrika Kusini na kufuata mapendekezo ya WHO ya mwezi Julai ikisema CAB-LA ina ufanisi mkubwa katika kupunguza maambukizi miongoni walio karibu vihatarishi vya kupata ugonjwa huo.

Nyasha Sithole wa Mtandao wa Agenda ya Maendeleo ya mtoto wa kike na mwanamke Afrika (DAWA) alisema, kuongeza kasi ya kuzuia VVU kwa wasichana na wanawake vijana kunahitaji upanuzi juu ya njia zinazopatikana.

“Nimefurahi na kujivunia kujua kuwa nchi yangu imeidhinisha matumizi ya CAB-LA. Hii itachangia mfuko wetu wa zana za kuzuia VVU ambazo zinatufanyia kazi kama wasichana na wanawake nchini Zimbabwe," amesema.

Credits: Mwananchi
Zimbabwe ya kwanza Afrika kuidhinisha sindano ya kuzuia Ukimwi (CAB-LA) Zimbabwe ya kwanza Afrika  kuidhinisha sindano ya kuzuia Ukimwi (CAB-LA) Reviewed by Zero Degree on 10/26/2022 04:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.