Loading...

Jumamosi tunaenda kutafuta pointi 3 - Ali Kamwe

Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe.

Ali Kamwe amewataka mashabiki wa klabu ya Yanga kuelekeza akili zaidi kwenye kupata alama tatu za mchezo wao dhidi ya Simba SC zaidi ya kufikiri zaidi kupata mabao mengi katika mchezo huo dhidi ya wapinzani wao wa jadi.

“Hizo hadithi ambazo mnazo kwenye magroup ya WhatsApp kwamba tunakwenda kumpiga mtu 20 nawaomba tuzibadilishe, naomba tuchukue focus ya kuchukua alama 3, hatutakuwa mabingwa kwa kumpiga Simba 100 tutakuwa mabingwa kwa kuwa na alama nyingi zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili.

“Novemba tano tulienda na ajenda ya alama tatu bahati nzuri kwetu wakachukua kiganja, jumamosi tunaenda kutafuta alama tatu ila wakajichanganya wakaamka vibaya tutalaumiana,” Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe.
Jumamosi tunaenda kutafuta pointi 3 - Ali Kamwe Jumamosi tunaenda kutafuta pointi 3 - Ali Kamwe Reviewed by Zero Degree on 4/15/2024 03:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.