Loading...

Mo Dewji, viongozi Simba SC wafanya kikao kizito

Rais wa Heshima Klabu ya Simba SC Mohammed Dewji akiongoza kikao na viongozi wa Simba.

Rais wa Heshima Klabu ya Simba SC Mohammed Dewji amefanya kikao na viongozi kujua changamoto zinazoikabili na kuzitatua timu hiyo kwa sasa.

Rais wa Heshima Klabu ya Simba SC Mohammed Dewji.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Mo Dewji ameandika:

“Nimefanya kikao na viongozi wa Simba SC kujua changamoto zipo wapi na namna ya kuzitatua. Kikao kimeenda vizuri. WanaSimba tusife moyo, tuendele kushirikiana.”

Baadhi ya Viongozi walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi Simba Salim Abdallah Muhene (Try Again), Mwenyekiti wa zamani Simba Swedi Nkwabi na Mshauri wa Mo Dewji, Crescentuis Magori.

Mwenyekiti wa Bodi Simba Salim Abdallah Muhene (Try Again), (Wa kwanza kulia) akizungumza jambo kwenye kikao hicho.
Mo Dewji, viongozi Simba SC wafanya kikao kizito Mo Dewji, viongozi Simba SC wafanya kikao kizito Reviewed by Zero Degree on 4/15/2024 02:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.