Makonda atinga Makao Makuu ya CCM Dodoma kuhojiwa na Kamati ya Maadili
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewasili kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili.
Makonda ameitikia wito wa kufika mbele ya kamati hiyo kwa barua aliyoandikiwa Aprili 16, 2024 huku sababu za kuitwa kwake zikiwa hazijawekwa wazi.
Awali, Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 kabla ya kusogezwa mbele na kupangwa kufanyika leo Jumatatu, Aprili 22, 2024.
Gazeti la Mwananchi ambalo limeweka kambi kwenye ofisi hizo limeshughudia Makonda akiwasili eneo hilo saa 3:15 asubuhi akiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 ya rangi ya kijivu. Hata hivyo, tofauti na siku zingine leo ulinzi kwenye ofisi hizo umeimarishwa zaidi.
Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
Makonda atinga Makao Makuu ya CCM Dodoma kuhojiwa na Kamati ya Maadili
Reviewed by Zero Degree
on
4/22/2024 08:50:00 AM
Rating:
