Sugu, Msigwa kivumbi na jasho kuwania uenyekiti
NI ‘kivumbi’ cha watia nia kwenye nafasi ya Uenyekiti Kanda ya Nyasa kuelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa Kanda mbalimbali za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), unaoendelea sasa.
Tofauti na ilivyo kwenye kanda mbalimbali za chama hicho ambazo zinatarajia kufanya uchaguzi huo Mei, mwaka huu, Kanda ya Nyasa inaonekana kuwa na ushindani mkali kuliko nyingine kutokana na wafuasi wa wagombea hao kuwa na mbwembwe nyingi ikiwamo majibizano kwenye mitandao ya kijamii kila upande ukionyesha na ushawishi wa kushinda.
‘Vigogo’wawili’ machachari wa chama hicho, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na Peter Msigwa, ndio wanaotia nia ya kuwania nafasi hiyo, huku wafuasi wao wakiwa na sare zenye picha na maneno zikiwapigia debe wagombea wao.
Sugu anagombea kwa mara ya kwanza, lakini Msigwa anapambana kutetea nafasi hiyo kwa kuwa mpaka sasa ndiye mwenyekiti wa kanda hiyo.
Duru za siasa zinaeleza kuwa Sugu ndiye Mbunge aliyeshinda kwa kura nyingi uchaguzi mkuu wa 2015 kwa kupata kura 97,675 huku mpinzani wake akipata 46,894.
Wote kwa nyakati tofauti, walijinasibu kwamba wameamua kufanya hivyo kutokana na shinikizo la wafuasi wao ambao ndio wanachama na wapiga kura wao.
Jana vigogo hao kwa nyakati tofauti, walirejesha fomu huku kila upande ukionyesha mbwembwe kwa mamia ya wafuasi wao wanaowaunga mkono ambao waliwasindikiza kurejesha fomu hizo.
Msigwa akiwa na kundi kubwa la wafuasi wake alirejesha fomu kwa ‘staili’ akiwa amenyanyuliwa juu na wafuasi wake hao huku wakiimba nyimbo za dini.
Mmoja wa wafuasi wa Msigwa aliyekuwa akiongoza msafara wakati kiongozi wao akirudisha fomu hiyo, alisikika akisema wafuasi hao walitoka katika mikoa mitano ya kanda hiyo ambao pia ni wapiga kura.
Kadhalika, Sugu na kundi kubwa la wafuasi wake walimsindikiza na baada ya kurudisha fomu hiyo alisema ameamua kubeba jukumu hilo baada ya kusukumwa na wanachama waliotaka mabadiliko kwenye kanda hiyo.
“Kwa nafasi yangu, yale niliyoyafanya kwenye chama, rekodi ya kazi zangu huko nyuma, nikaona nitakuwa mbinafsi kama nitagoma juu ya heshima ambayo wenzangu mmenipa kwa sasa katika kuelekea uchaguzi huo, mmenipa heshima kubwa na mwanzo mliposema tuko pamoja nikajua ni utani maana mjini ukiambiwa tuko pamoja ukigeuka nyuma huoni mtu,” amesema Sugu.
“Lakini kufikia jana (juzi), kwenye kikao chetu ambapo mlijikusanya kama viongozi na wapigakura na mkasema kwamba mje tuonane kuhakikisha kwamba mko pamoja na mimi, tena kutoka mikoa yote mitano, kwa kweli niliamini, kwa hiyo nawashukuru sana.”
“Niko tayari kufanya kazi hii kwa uaminifu mkubwa kwa sababu sijaianza leo, leo ni kurudisha fomu tu, kampeni hazijaanza, yale mengi yanayohusiana na kujieleza kwamba tutafanya nini nitakuja kuyaeleza kwenye maeneo yenu wakati utakapofika kwa sababu nitazunguka katika majimbo yote 31 katika mikoa mitano kuja kuzungumza na ninyi uelekeo wetu wa mbele ili kuakisi kiu ya mabadiliko mnayoyataka katika Kanda ya Nyasa,” amesema Sugu.
Aidha, ametaja vipaumbele vyake endapo atachaguliwa katika nafasi hiyo kuwa ni pamoja na kurejesha kanda hiyo kwa wanachama na siyo kujifungia ndani na kufanya uamuzi peke yake na kupuuzia maoni ya wanachama.
Kipaumbele cha pili amesema ni kwenda kusimamia makakati wa kusaka ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 pamoja na kusimamia programu ya ‘CHADEMA Digital’.
Uchaguzi huo wa kanda unafanyika baada ya kumalizika wa wilaya na mikoa na baadae utatangazwa uchaguzi wa mwenyekiti taifa.
Wengine wanaotajwa kutia nia ya kuchuana katika uenyekiti katika kanda mbalimbali kwenye mabano ni Ezekiel Wenje, John Heche na John Pambalu (Kanda ya Victoria), Boniface Jacob na Baraka Mwago (Kanda ya Pwani), Gaston Shundo na Dickson Matata (Kanda ya Magharibi).
Aidha, Aisha Luja na David Jumbe Kanda ya Kati wakati Kanda ya Kaskazini anayetajwa bado ni Godbless Lema pekee ambaye ndiye mwenyekiti.

Chanzo: IPPmedia
Sugu, Msigwa kivumbi na jasho kuwania uenyekiti
Reviewed by Zero Degree
on
4/22/2024 08:45:00 AM
Rating: