Mkuu wa majeshi ya ulinzi Kenya afariki dunia katika ajali ya helikopta
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Kenya Francis Ogolla amefariki.
Rais William Ruto ametangaza kifo cha Ogolla pamoja na maafisa wengine 9 wa jeshi huku wawili wakinusuruka.
Ogolla alifariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria pamoja na maafisa wengine kuanguka Kaben, Marakwet Mashariki siku ya Alhamisi.
Ogolla alichukua nafasi ya kuongoza jeshi mnamo Aprili 28, 2023.
Walioshuhudia walisema kuwa ilishika moto wakati wa kuanguka.
Eneo hilo lilizingirwa mara baada ya ajali hiyo.
Maafisa hao walikuwa wakichunguza eneo hilo kabla ya kutumwa kwa wanajeshi zaidi kukabiliana na wezi wa mifugo katika eneo hilo.
Helikopta hiyo ya jeshi la Anga la Kenya aina ya Huey ilikuwa imetoka katika shule ya msingi ya eneo hilo ilipoanguka na kuwaka moto.
Ogolla aliteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi katika mabadiliko katika jeshi, akichukua hatamu kutoka kwa mtangulizi wake Jenerali Robert Kibochi.
Kibochi alimkabidhi Ogolla kama Mkuu wa majeshi baada ya kufikisha umri wa kustaafu.
Siku tatu za maombolezo
Akitangaza kifo cha Jenerali Ogolla rais Ruto amesema kutakuwa na siku tatu za maombolezo kuanzia Ijumaa tarehe 19 Aprili ambapo bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kwa kipindi hicho . Rais alisema Ogolla alikuwa katika kaunti ya Elgeyo Marakwet kuwatembelea wanajeshi wanaoendesha oparesheni ya kupambana na wezi wa mifugo inayoitwa 'operesheni maliza uhalifu' na kukagua miradi ya ukarabati wa shule kadhaa za msingi katika eneo hilo .
Cc: BBC
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Kenya afariki dunia katika ajali ya helikopta
Reviewed by Zero Degree
on
4/18/2024 08:38:00 PM
Rating:
