Loading...

Aziz Ki ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu bara 2023/24


Licha ya Feitoto kupachika bao moja kwenye ushindi wa Azam jana, alishindwa kutwaa kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora. Hiyo ni baada ya kuzidiwa na kiungo wa Yanga, Azizi Ki ambaye alipachika mabao matatu wakicheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, na kuisaidia timu yake kuondoka na ushindi wa mabao 4-1.

Mabao hayo yamemfanya Aziz Ki kufikisha idadi ya mabao 21 akimuacha Feitoto kwa mabao mawili na kuongeza furaha kwa mashabiki wa Yanga ambao mapema wiki iliyopita walishuhudia timu yao ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo.

Mchuano wa kuwania tuzo hiyo ulikuwa mkali na kabla ya michezo ya jana wachezaji wote walikuwa na magoli 18 na hivyo kusubiri michezo ya mwisho kujua nani atakuwa kinara wa mabao msimu huu.


Mabao hayo matatu aliyofunga Aziz Ki yanamfanya kufikisha 'hat trick' mbili (mabao matatu katika mchezo mmoja) kwenye Ligi Kuu msimu huu ikitanguliwa na ile ya kwanza aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya Azam, Oktoba 23, mwaka jana.
Aziz Ki ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu bara 2023/24 Aziz Ki ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu bara 2023/24 Reviewed by Zero Degree on 5/29/2024 08:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.