Kijana atupwa jela miaka 30 kwa wizi wa simu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Lindi imemuhukumu Naimu Ally M’baruku maarufu Soggy mwenye umri wa miaka 20, Mkazi wa Mtaa wa Ndoro Manispaa ya Lindi kwenda Jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kunyang’anya simu aina ya TECNO SPARK 8 kwa kutumia silaha (panga).
Katika hatua nyingine Mahakama ya Wilaya ya Kilwa imemuhukumu Kamugisha Filbert Rugemalila (47) na Jamilu Swaibu Kichwabuti ( 25) wote Wakazi wa Dar es salaam kwenda jela kifungo cha miaka mitano kika mmoja kwa kosa la wizi (Vifaa mbalimbali kwa ajili ya kazi ya kuchukulia Video).
Kijana atupwa jela miaka 30 kwa wizi wa simu
Reviewed by Zero Degree
on
5/21/2024 09:39:00 AM
Rating:
