Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 21 Mei, 2024


Meneja wa Burnley Vincent Kompany, 38, ni miongoni mwa watu wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel huko Bayern Munich.

Newcastle wanaweza kumnunua Lloyd Kelly, 25, huku beki huyo wa timu ya taifa ya Uingereza akitarajiwa kuondoka Bournemouth kama mchezaji huru. (Fabrizio Romano)

Klabu ya Aston Villa inakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua tena mchezaji wa Luton Town na kiungo wa kati wa zamani wa Uingereza Ross Barkley kwa mkataba wa kudumu, miaka minne baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kujiunga kwa mkopo kutoka Chelsea. (Guardian)

Arsenal wanataka kusajili mshambuliaji kabla ya ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya, huku nyota wa klabu ya Newcastle United na Uswidi Alexander Isak, 24, na mshambuliaji wa Ajax na Uholanzi, Brian Brobbey, wakiongoza orodha hiyo.(Independent)


Klabu za Chelsea pamoja na Manchester United zote zimewasiliana na mkufunzi wa Ipswich Town Kieran McKenna, huku raia huyo wa Ireland Kaskazini akiwa katika harakati za kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino au Erik ten Hag. (Manchester Evening News)

Chelsea itadai ada ya pauni milioni 25 kwa mlinzi wa Uingereza Trevoh Chalobah, 24, ambaye anatarajiwa kuvutia vilabu kadhaa.

Aston Villa wako tayari kusikiliza ofa kwa mlinzi wa Brazil Diego Carlos, 31, huku wakitarajia kufuata sheria za faida na uendelevu.

Wolves itadai kiasi cha kuvunja rekodi ya klabu cha pauni milioni 60 kwa winga wa Ureno mwenye umri wa miaka 24 Pedro Neto, ambaye analengwa na Manchester City na Newcastle msimu wa joto. (Telegraph)

Mkufunzi wa Villa Unai Emery anataka kumsajili beki wa Barcelona na Uruguay Ronald Araujo, 25. (Sport)

Stoke wameonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Uingereza Conor Coady, 31, kutoka Leicester. (Teamtalk)

Leicester wanajiandaa kushindana na vilabu vya Ufaransa Lyon na Brest kumnunua fowadi wa Burkina Faso Mohamed Konate, 26, ambaye mkataba wake na klabu ya Urusi Akhmat Grozny unamalizika msimu huu. (Football Insider)

Meneja wa Tottenham Ange Postecoglou ameiomba klabu hiyo takriban wachezaji watatu wapya msimu huu wa joto. (ESPN)

Manchester United wanavutiwa na mlinzi wa Everton Muingereza Jarrad Branthwaite, 21, na The Toffees wanaweza kumnunua beki wa kati wa Galatasaray na Colombia Davinson Sanchez, 27, kuziba nafasi yake. (Caught Offside)


Tottenham wako tayari kumuuza mlinzi wa Brazil Emerson Royal, 25, huku Juventus , AC Milan na Bayern Munich zikiwa na hamu ya kumnunua. (Givemesport)

Rais wa Corinthians Augusto Melo atasafiri hadi Uingereza wiki ijayo kuzungumza na vilabu kuhusu uwezekano wa kuuzwa kwa mshambuliaji wa Brazil Wesley mwenye umri wa miaka 19. (Globo Esporte)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 21 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 21 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/21/2024 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.