Loading...

Ligi kuu bara msimu wa 2023/24 kufikia tamati leo


Ligi Kuu Tanzania Bara inafikia tamati leo kwa nyasi za viwanja nane kuwaka moto. licha ya kujulikana bingwa wa msimu huu lakini vita vikali vipo kutafuta mshindi wa pili katika ya Azam FC na Simba.

Michezo ya leo ni mabingwa wapya wa msimu huu Yanga, kukamilisha ratiba dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi. Simba watawakaribisha JKT Tanzania Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Mechi zingine ni Geita Gold FC wakiwa nyumbani Uwanja wa Nyankumbu akimkaribisha Azam FC, Namungo FC dhidi ya Tabora United, Majaliwa Stadium, Lindi, Singida Fountain Gate FC dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa CCM Kirumba.

Coastal Union dhidi ya KMC FC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mashujaa FC watakuwa nyumbani ikiwakaribisha Dodoma Jiji FC. Lake Tanganyika, Kigoma na Ihefu FC dhidi ya Mtibwa Sugar ambaye tayari ameshuka daraja.

Katika michezo ya leo kuna kuwania nafasi ya pili lakini vita vikali ipo katika kuwania tuzo ya ufungaji bora kati ya viungo washambuliaji wawili Stephen Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wote wakiwa wamefunga mabao 18.

Lakini kuna timu ambazo zinajinasua kushuka na kutafuta nafasi ya kucheza Play Off ambapo Geita Gold FC ambao wako nafasi ya 15 ya pili kutoka chini anakutana na Azam FC ambayo nayo ipo katika vita vya kutafuta nafasi ya pili ili kwenda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Matumaini ya Simba kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao yamebebwa na Geita Gold FC ambaye akimfunga Azam FC, anaenda kucheza Play Off na kuwapa nafasi timu ya Wekundu wa Msimbazi kwenda kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa. 

Chanzo: Nipashe
Ligi kuu bara msimu wa 2023/24 kufikia tamati leo Ligi kuu bara msimu wa 2023/24 kufikia tamati leo Reviewed by Zero Degree on 5/28/2024 08:38:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.