Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Mei, 2024

Emerson Royal, 25

AC Milan wanavutiwa na beki wa Brazil na klabu ya Tottenham Emerson Royal mwenye umri wa miaka 25. (Gianluca di Marzio)

Manchester United wamezungumza na kocha wa zamani wa Brighton Roberto de Zerbi kuhusu uwezekano wa kumrithi Erik ten Hag kama meneja. (Guardian)

Lakini United wanafikiria kumbakisha Ten Hag kama mkufunzi wao. (Manchester Evening News)

Mkufunzi wa Ipswich Kieran McKenna anakaribia kusaini mkataba mpya wa kudumu licha ya Chelsea, Manchester United na Brighton kumtaka. (Athletic)

Paris St-Germain wako tayari kumenyana na Manchester City na Arsenal kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle na Brazil Bruno Guimaraes, 26, mwenye thamani ya pauni milioni 100. (Goal)

Kiungo wa kati wa zamani wa England Adam Lallana, 36, yuko kwenye mazungumzo ya kurejea Southampton kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake wa Brighton utakapokamilika mwezi ujao. (Telegraph)

Chelsea wanafikiria kumenyana na Newcastle kumnunua mlinzi wa Uingereza Tosin Adarabioyo, 26, ambaye atakuwa mchezaji huru mkataba wake utakapokamilika Fulham mwezi ujao. (The i)

Klabu ya Southampton itajaribu kuwasajili winga wa West Ham Muingereza Flynn Downes, 25, na winga wa Newcastle wa Scotland Ryan Fraser mwenye umri wa miaka 30 kwa mikataba ya kudumu baada kucheza kwa mkopo msimu uliopita. (Daily Echo)

Leicester huenda wakamlenga kocha wa West Brom Carlos Corberan iwapo Enzo Maresca atajiunga na Chelsea. (Talksport)

Newcastle wanafikiria kuwasilisha dau la pauni milioni 20 kumnunua mlinda mlango wa Burnley mwenye umri wa miaka 21 wa Uingereza James Trafford. (Mail)

Liverpool pia wanamtaka Trafford, huku kipa wao wa Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 25, akitafuta kuondoka katika klabu hiyo.


Manchester United wanatarajia kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 32, kujiungana na klabu ya ligi kuu ya Saudia katika msimu huu wa joto na wako tayari kumuuza. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Uholanzi Xavi Simons, 21, anataka kujiunga na Barcelona licha ya kuwaniwa na Leipzig, Bayern Munich, Chelsea, Manchester United na Newcastle.

Aston Villa hawana nia ya kumnunua beki wa Barcelona Clement Lenglet, 28. Mfaransa huyo amemaliza mkopo wa msimu mzima katika klabu hiyo ya Villa Park. (Mundo Deportivo)

Liverpool na Chelsea ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu zinazovutiwa na mshambuliaji wa Leeds United Mholanzi Crysencio Summerville, 22. (Kioo)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku

Mkufunzi mpya wa Napoli Antonio Conte anataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 25, kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, ambaye anatarajia kujiunga na timu ya Ligi Kuu ya England. (Corriere Della Sera)

Klabu ya Norwich City inamtaka beki wa kushoto wa Denmark Martin Frese, 26, ambaye mkataba wake na Nordsjaelland unakaribia kuisha. (Bold)

Real Madrid wako tayari kutoa zaidi ya £25m kwa ajili ya mlinzi wa Lille Mfaransa Leny Yoro, 18, ambaye pia anahusishwa na Paris St-Germain na Liverpoool. (Foot Mercato)

Kocha wa zamani wa Bayern Munich na Ujerumani Hansi Flick atasaini mkataba wa miaka miwili kuwa mkufunzi wa Barcelona siku ya Jumatano. (Fabrizio Romano)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/28/2024 09:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.