Loading...

Muhimu kwetu ni kushinda na kufikia malengo yetu


Mapema kuelekea mchezo wa Simba dhidi ya JKT, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda, alisema maandalizi ya mchezo wa leo yapo vizuri na muhimu kwao kupata matokeo ya ushindi.
“Naweza kesho (leo), ndio tunafunga shule kwa sababu tunamaliza mechi ya mwisho wa kumaliza ligi ni muhimu kwetu kushinda na kufikia malengo yetu, mechi hii ni ya maamuzi na kila mmoja ana mahitaji yake. Itakuwa mechi inayohitaji umakini na dakika 90 tutapata uamuzi.

Licha ya kufanya vizuri lakini wachezaji wangu wapo vizuri kisaikolojia na wanafahamu umuhimu wa kushinda mchezo wa leo,” alisema Mgunda.

Kocha Msaidizi wa JKT, George Mketo alisema wamejiandaa kwa mchezo wa leo wanaimani utakuwa mchezo mgumu kulingana na mahitaji ya kila timu kwa upande wao kupata matokeo mazuri.

Alisema wanafahamu ubora wa Simba hasa katika maeneo ya pembeni na kati kwa kuwa na nguvu na wanaenda kupambana kutafuta matokeo chanya na kupata alama.

“Simba ina wachezaji wakubwa na wakomavu na tunaenda kucheza kwa namna mbili kukabilian na ubora wa wapinzani wetu na kufanikiwa kuvuna alama muhimu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusalia katika ligi,” alisema Mketo.
Muhimu kwetu ni kushinda na kufikia malengo yetu Muhimu kwetu ni kushinda na kufikia malengo yetu Reviewed by Zero Degree on 5/28/2024 11:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.