Loading...

Makamba ataja vipaumbele 5 katika mwaka wa fedha 2024/25

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imetaja vipaumbele vitano katika mwaka wa fedha 2024/25.
Moja ya vipaumbele hivyo ni kuratibu utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ili kuchochea uwekezaji, utalii na biashara na kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa maendeleo ya nchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, alibainisha hayo jana bungeni wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka 2024/25.

Makamba alisema ili kufanikisha vipaumbele hivyo, aliliomba bunge kuidhinisha Sh. bilioni 241.09, kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 229.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. bilioni 11.6 ni kwa ajili ya maendeleo.

Kipaumbele kingine ni kuongeza ushawishi wa Tanzania kwa nchi zingine katika masuala mtambuka kwenye jumuiya na mashirika ya kikanda ya kimataifa.

“Kushiriki kwenye jitihada kikanda na kimataifa za kudumisha amani, ulinzi na usalama na kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi, kuimarisha utawala bora na rasilimali watu pamoja na kutekeleza miradi ya ujenzi, ununuzi na ukarabati wa majengo ya ofisi, makazi ya watumishi na vitega uchumi katika balozi za Tanzania na makao makuu.” alisema Makamba
Makamba ataja vipaumbele 5 katika mwaka wa fedha 2024/25 Makamba ataja vipaumbele 5 katika mwaka wa fedha 2024/25 Reviewed by Zero Degree on 5/29/2024 09:54:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.