Loading...

Tanzania inaunga mkono uamuzi wa SADC - Majaliwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaunga mkono uamuzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) juu ya kuongeza mbinu za uvunaji wa maji, udhibiti wa mafuriko na miundombinu ya kuhifadhi maji hayo ili yatumike wakati wa ukame ama kiangazi kuzuia mafuriko msimu wa mvua nyingi.

Waziri Mkuu amesema hayo leo (Jumatatu, Mei 20, 2024) wakati akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kuhusu athari za mvua za El Nino. Ameshiriki mkutano huo kwa njia ya mitandao kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.


“Tanzania inaunga mkono uamuzi huo na inasisitiza Sekretariet ya SADC kuongeza misaada kwa nchi wanachama katika ujenzi wa mabwawa ya kutunza maji ambayo yatatumika katika vipindi vya ukame na kiangazi pamoja na kuzuia mafuriko katika vipindi vya mvua,” amesema Majaliwa.




Tanzania inaunga mkono uamuzi wa SADC - Majaliwa Tanzania inaunga mkono uamuzi wa SADC - Majaliwa Reviewed by Zero Degree on 5/20/2024 08:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.