Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 24 Mei, 2024

Mlinda mlango wa Manchester City na Brazil Ederson

Manchester City ya Pep Guardiola haitamzuia mlinda lango wa Brazil Ederson ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anataka kuhamia Saudi Arabia, lakini masharti yanapaswa kuwa sawa kwao juu ya uhamisho wowote.

Klabu ya Liverpool wameelekeza mawazo yao kwa winga wa Leeds Mholanzi Crysencio Summerville, 22, baada ya kuamua kumnunua winga wa Newcastle na England Anthony Gordon, 23. (90 Min)

Newcastle United wanawania wachezaji wawili wa Uingereza, huku Thomas Tuchel akiwa mgombea anayeongoza kuchukua mikoba huko Manchester United.

Winga wa Brazil Willian, mwenye umri wa miaka 35, amepewa ofa kutoka Saudi Arabia ili azingatie kwani mkataba wake na Fulham unakaribia kuisha.

Klabu ya Newcastle United wanatumai kusajili wachezaji wawili wa kimataifa wa timu ya taifa ya Uingereza huku mshambuliaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin, mwenye umri wa miaka 27, na mshambuliaji wa West Ham Jarrod Bowen, pia mwenye umri wa miaka 27, wakiwa kwenye rada yao.(Telegraph)

Newcastle wanataka karibu pauni milioni 200 kumnunua mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal. (Mirror)

Thomas Tuchel, ambaye yuko huru baada ya kuondoka Bayern Munich, ndiye mgombea anayeongoza kuchukua mikoba ya Manchester United ikiwa klabu hiyo ya Old Trafford itamfukuza Erik ten Hag baada ya fainali ya Kombe la FA. (Guardian)

Meneja wa klabu ya Ipswich Town Kieran McKenna yuko tayari kuchukua mikoba ya kukinoa Manchester United iwapo Ten Hag ataondoka. (Manchester Evening News)

Klabu ya Brighton wana uhakika wa kuipiku Chelsea katika kumwajiri McKenna lakini wanaweza kujaribu kumrejesha meneja wa zamani Graham Potter iwapo watashindwa kufanya hivyo.(Times)

Klabu ya Chelsea wako tayari kuomba nafasi kwa Leicester City iliyopanda daraja iwaruhusu kuzungumza na Enzo Maresca kuhusu nafasi yao ya ukocha. (Sports)

Bayern Munich wanamfuatilia beki wa England na Manchester City John Stones, mwenye umri wa miaka 29. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 28, pia analengwa na Bayern. (Sun)

Burnley wanaomba fidia ya £17m kutoka kwa Bayern ili kumruhusu meneja Vincent Kompany kuchukua mikoba katika klabu hiyo ya Ujerumani. (Sky Sports Ujerumani)

Michael Olise, 22

Manchester United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kuinasa sahihi ya winga wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ufaransa Michael Olise, 22. (Football Transfers)

Klabu ya Aston Villa wanafikiria kusitisha mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 31. (Givemesport)

Winga wa Nottingham Forest na Uingereza Callum Hudson-Odoi, 22, anatarajiwa kulengwa na Tottenham. (Guardian)

Ajax na Feyenoord wanavutiwa na winga wa Chelsea Omari Hutchinson, mwenye umri wa miaka 22, ambaye aliichezea Ipswich kwa mkopo msimu uliopita. (Football London)

Mchezaji wa klabu ya Stoke Souleymane Sidibe, mwenye umri wa miaka 17, anaweza kuhama msimu huu huku Brighton , Chelsea , Monaco na Juventus wakimtaka kiungo huyo wa kati wa Ufaransa. (Foot Mercato)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 24 Mei, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 24 Mei, 2024 Reviewed by Zero Degree on 5/24/2024 08:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.