Loading...

Usyk atwaa ubingwa wa dunia baada ya kumshinda Tyson Fury

Usyk alirudi kwenye shindano katika nusu ya pili ya pambano

Tyson Fury alishindwa kwa pointi nchini Saudi Arabia huku Oleksandr Usyk akiwa bingwa wa kwanza wa ndondi za uzani mzito zaidi kushikilia mikanda minne duniani.

Katika usiku uliosheheni ujuzi wa kila aina kutoka kwa mabondia hao Tyson Fury alianza vyema mechi hiyo lakini akaokolewa na kengele katika raunndi ya tisa kutokanna na kichapo cha Usyk.

Akiwa katika hali ya kusubiri kadi za matokeo kusomwa, Fury alionekana kushawishika kupata ushindi kabla ya kadi hizo kumpatia ushindi Usyk.

Kadi za matokeo zilisomeka 115-112 na 114-113 kwa raia wa Ukraine, huku jaji wa tatu akifunga 114-113 kwa Fury.

Ilimaanisha Fury, 35, alipoteza kwa mara ya kwanza katika taaluma ya miaka 16. Atapata fursa ya kulipiza kisasi kwa mechi ya marudiano iliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

"Ninaamini alishinda raundi chache, lakini nilishinda nyingi," Fury alinukuliwa akisema kwenye jukwaa hilo.

"Ilikuwa moja ya maamuzi mabaya zaidi katika historia ya ndondi. Nitarejea."

Usyk anachukua mkanda wa WBC kutoka kwa Fury, ili kuongeza kwenye mkusanyiko wake wa WBA, WBO na IBF.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 bado hajashindwa na anakuwa bondia wa kwanza katika takriban miaka 25 kusimama kidete kama bingwa pekee wa dunia wa uzito wa juu.

"Asante sana kwa timu yangu. Ni fursa kubwa kwa familia yangu, kwangu, kwa nchi yangu. Ni wakati mzuri, ni siku nzuri," Usyk alisema.

"Ndiyo, bila shaka. Niko tayari kwa mechi ya marudiano."

Usyk ashinda pambano la kihistoria

Usyk sasa anashikilia mataji ya uzito wa juu ya WBA, IBF, WBO na WBC

Tyson Fury hakuwahi kupoteza pambano la kulipwa kwa miaka 16.

Usyk - bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa cruiserweight - alishinda katika pambano ambalo linamuweka katika historia ya ndondi kuwa mmoja wa nguli wa mchezo huo duniani.

Baada ya kukosekana kwa mbwembwe na kelele uwanjani kwa mapigano ya yaliofanyika mapema, takriban mashabiki 20,000 waliojumuisha sura maarufu kama Cristiano Ronaldo walijipata wakishangilia ghafla.

Usyk - anayefanana na shujaa – aliingia katika jukwaa hilo akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni ya Ukraine ya kijani kibichi, macho yake yakilimwilika jukwaa hilo.

Kinyume na ukali wa Usyk, Fury ambaye ni mcheshi aliimba na kucheza ngoma ya Bonnie Tyler Holding Out For A Hero.

Mechi ikianza Fury alielekea katika kona ya mpinzani wake na kuanza kummiminia makonde mazito hatua iliowafurusha mashabiki 2,500 wa Uingereza waliosafiri.

Huku mabingwa hao wawili wakikabiliana katikati ya jukwaa , mechi ilibadilika na Usyk akaanza kumshambulia mpinzani wake na kumrudisha nyuma kwa ngumi nzito.

Hatahivyo Fury aliyekuwa akitabasamu wakati wote huo alionesha ushupavu wake na kumaliza raundi ya kwanza licha ya Usyk kumpata ngumu ya kushoto na kumrudisha nyuma kwa kasi.

Mwenye tabasamu na shupavu alipitia raundi ya kwanza. Hata wakati Usyk alipotua ndoano thabiti ya kushoto na kumuunga mkono kwenye kona, Mfalme wa Gypsy alicheka kwa ghadhabu.

Fury alijibu kwa njia mbili za juu zenye sura chungu kwa Usyk katikati ya dakika ya pili.

Urefu na faida ya kufikia ya Fury ilikuwa inaleta fumbo nyingi sana kwa Usyk kutatua, au ndivyo ilionekana.

Usyk alirudi kwenye shindano katika nusu ya pili ya pambano.

Bondia huyo amekuwa akianza mapigano yake kwa kasi ya chini hatua ambayo imesababisha kujeruhiwa mara nyingi.

Lakini alirudi kwa kishindo katika raundi ya tisa .

Huku Lennox Lewis, bingwa wa mwisho ambaye alishikilia mikanda mitatu katika uzani mzito zaidi duniani, na mabingwa wenzake wa zamani Larry Holmes na Evander Holyfield wakitazama pigano hilo, Usyk hatimaye alionyesha umahiri wake.

Baada ya msururu wa makonde ya kushoto kulia dhidi ya, Fury aliyekuwa akirudi nyuma na kuduwaa, refa aliingilia kati na kumzuia Usyk kuendeleza mashambulizi yake – ikiashiria knock out.

Akionekana kutetereka na kutegemea kamba za ulingo , refa alihesabu hadi 10 kabla ya kengele.

Hii haikuwa mechi ya kuchosha, ya kimbinu, kama ilivyotabiriwa na baadhi ya wachambuzi bali pigano lililosheheni makabiliano kutoka kwa mabondia wote wawili.

Ngumi nyengine ya kushoto kutoka kwa Usyk ilimpata Fury katika raundi ya 11.

Wawili hao walisalimiana kabla ya kuanza kwa raundi ya 12 huku mashabiki wakihisi kwamba mechi bado haijakamilika.

Lakini ilikuwa Usyk ambaye alionekana kumaliza raundi ya mwisho akiwa mchangamfu hali iliomfanya kushinda mechi hiyo.

Usyk awika mbele ya Tyson Fury

Oleksandr Usyk ndiye bingwa wa kwanza wa dunia wa uzani wa juu ambaye hajashindwa katika enzi ya mikanda minne

Pigano lisilo na mvuto la Oktoba dhidi ya Francis Ngannou liliwaacha wengi wakijiuliza ikiwa siku bora za Fury zilikuwa zimepita.

Lakini alikuwa mshindani mzuri na anayefaa na maoni yoyote dhidi yake yake kwamba alikuwa amepitwa na wakati yalizikwa katika kaburi la sahau alipodhibiti sehemu za mapema za mechi hiyo.

Fursa yake ya kuwa bingwa anayeshikilia mataji manne duniani huenda isije tena hivi karibuni.

Mechi ya marudiano inatarajiwa mwezi Oktoba lakini hakuna uwezekano kuwa itashirikisha mikanda yote minne - IBF inapanga kumvua Usyk taji hilo kwani hayuko tayari kukabiliana na mpinzani wao wa lazima.

"Tutarudi, napumzika. Ninaamini nilishinda pambano lakini sitakaa hapa kulia na kutoa visingizio. Tutapigana tena," Fury aliongeza.

Taji la dunia la uzito wa juu linazingatiwa na wapenzi wa ndondi kama tuzo kuu zaidi, inayotamaniwa zaidi katika mchezo, na mpiganaji huyo mzaliwa wa Crimea aliacha ulingo akiwa amejifunga mikanda yote minne kwenye fremu yake ya futi 6 na inchi 3.

BBC
Usyk atwaa ubingwa wa dunia baada ya kumshinda Tyson Fury Usyk atwaa ubingwa wa dunia baada ya  kumshinda Tyson Fury Reviewed by Zero Degree on 5/19/2024 11:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.