Loading...

Utabiri mwingine wa kimbunga, TMA imetoa tahadhari


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla ya kuanza kupungua nguvu.

Aidha, kutokana na umbali kutoka nchini, kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja katika kusababisha ongezeko la mvua nchini. Hata hivyo vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi.

Kufuatia uwepo wa Kimbunga IALY, watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.
Utabiri mwingine wa kimbunga, TMA imetoa tahadhari Utabiri mwingine wa kimbunga, TMA imetoa tahadhari Reviewed by Zero Degree on 5/17/2024 02:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.