Loading...

Wakandarasi wa umeme zingatieni weledi - DC Kheri James

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komred Kheri James

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komred Kheri James amewataka wakandarasi wenye leseni za umeme Mkoani Iringa kufanya kazi kwa weledi katika kazi zao.

Ameyasema hayo tarehe 17 Mei 2024 Mkoani Iringa wakati wa kufungua kikao kilicholikutanisha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Iringa na wakandarasi wenye leseni za umeme Mkoani Iringa, kilichokuwa na lengo la kujadili mikakati ya kuboresha huduma kwa mteja.

“Wakandarasi wa umeme ni vyema mkazingatia weledi wakati mnatekeleza majukumu yenu ili kuhakikisha mteja anapata huduma yenye viwango,” amesema Komred Kheri James.

Ameongeza kuwa ubora wa kazi wanazofanya wakandarasi ni muhimu kwani hujenga sifa nzuri ya TANESCO na wakandarasi kwa mteja, huku akisisitiza kutoruhusu vishoka (watu wasio waaminifu) kuingilia fani yao kwani inaharibu taswira ya kazi yao kwa wateja.


“Pia, wananchi wengi hawana vipato vikubwa hivyo gharama za kuweka mtandao wa nyaya kwenye nyumba (waring) mnazowatoza jitahidini ziwe na unafuu ilikuwasadia kumudu gharama hizo,” amesisitiza Komred Kheri James.

Komred Kheri James ameeleza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inazalisha umeme wa kutosha, na inakamilisha kazi ya usambazaji wa umeme.


Akizunguzia Wilaya ya Iringa, Komred Kheri James ameeleza kuwa Serikali imekamilisha zoezi la kusambaza umeme katika vijiji vyote na sasa imetenga kiasi cha shilingi bilioni 26 ili kwenda kuanza hatua ya vitongoji.

Nae, Kaimu Meneja wa Mkoa wa Iringa Mhandisi Herman Bucheye anasema kuwa kukutana na wakandarasi wenye leseni za umeme mkoani humo ni kuwakumbusha wajibu wao, kupokea maoni na kujibu hoja zao ili kuhakikisha mteja anapata huduma nzuri.



Wakizungumza mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho, wakandarasi wameipongeza TANESCO na wameahidi kuongeza weledi na kushirikiana na TANESCO.
Wakandarasi wa umeme zingatieni weledi - DC Kheri James Wakandarasi wa umeme zingatieni weledi - DC Kheri James Reviewed by Zero Degree on 5/18/2024 02:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.