Loading...

Kituo cha Umeme Nyakanazi chaimarisha upatikanaji wa umeme Bukombe, Mbogwe, Biharamulo na Chato


Serikali imesema kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi mkoani Kagera imepelekea kutenganisha matumizi ya umeme katika wilaya za Bukombe, Mbogwe, Biharamulo na Chato jambo ambalo limesaidia kila wilaya kujitegemea na pia kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme katika Wilaya ya Biharamulo.

Naibu waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa katika Wizara ya Nishati na Waheshimiwa Wabunge akiwemo Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa.


Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa TANESCO inaendelea na matengenezo ya kuimarisha miundombinu ya kusafirishia na kusambazia umeme katika Wilaya ya Biharamulo ili kuwe na umeme wa uhakika.
Kituo cha Umeme Nyakanazi chaimarisha upatikanaji wa umeme Bukombe, Mbogwe, Biharamulo na Chato Kituo cha Umeme Nyakanazi chaimarisha upatikanaji wa umeme Bukombe, Mbogwe, Biharamulo na Chato Reviewed by Zero Degree on 6/05/2024 05:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.