Loading...

Rasmi: Chelsea imethibitisha kuwa Enzo Maresca ndiye kocha mkuu wa klabu hiyo


Chelsea wamemteua mkufunzi wa Leicester Enzo Maresca kama kocha wao mpya kwa kandarasi ya miaka mitano na chaguo la nyongeza ya mwaka.

Muitaliano huyo anachukua nafasi ya Mauricio Pochettino, ambaye aliondoka kwa makubaliano tarehe 21 Mei baada ya msimu mmoja tu Stamford Bridge.

Maresca, 44, alichukua jukumu la kuinoa Foxes mnamo Juni 2023 na kuwaongoza kuchukua ubingwa msimu uliopita.

"Kujiunga na Chelsea, moja ya klabu kubwa duniani, ni ndoto kwa kocha yeyote," alisema. "Ndio maana nimefurahishwa sana na fursa hii.

"Ninatarajia kufanya kazi na kundi la wachezaji na wafanyikazi wenye vipaji ili kukuza timu ambayo inaendeleza utamaduni wa mafanikio wa klabu na kuwafanya mashabiki wetu wajivunie."

Maresca, ambaye ataanza kazi yake mpya Julai 1, ni kocha wa Chelsea katika kipindi cha miaka mitano na wa nne tangu mwekezaji Mmarekani Todd Boehly na kampuni ya hisa ya Clearlake Capital kuinunua klabu hiyo Mei 2022.
Rasmi: Chelsea imethibitisha kuwa Enzo Maresca ndiye kocha mkuu wa klabu hiyo Rasmi: Chelsea imethibitisha kuwa Enzo Maresca ndiye kocha mkuu wa klabu hiyo Reviewed by Zero Degree on 6/04/2024 06:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.