Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 9 Juni, 2024

Newcastle wawasilisha dau la kumnunua kipa James Trafford wa Burnley

Newcastle wamewasilisha dau la pauni milioni 16 kwa Burnley kumnunua mlinda mlango wa Uingereza James Trafford, 21, lakini Clarets wanataka pauni milioni 20.

Kocha wa Fulham Marco Silva anaweza kulengwa na Nottingham Forest iwapo meneja wao Nuno Espirito Santo ataondoka kwenye Uwanja wa City. (Mail)

Manchester United wanatarajia kukamilisha dili la kumnunua beki wa Everton, Jarrad Branthwaite kabla ya Juni 30 baada ya kiongo huyi kuachwa nje ya kikosi cha England cha Euro 2024. (Liverpool Echo)

Klabu ya Manchester United wanajiandaa kuwasilisha ofa ya pili kwa kiungo wa Benfica Joao Neves, 19, baada ya ofa ya awali ya £51m kukataliwa. (A Bola)

Manchester City hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez

Klabu ya Manchester City wanataka kumbakisha mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 24 na hawatapokea ofa zozote za mkopo kwa mchezaji huyo. (Fabrizio Romano)

Atletico Madrid wamekuwa wakihusishwa na Alvarez lakini rais wa klabu yao Enrique Cerezo anasema haamini kuwa mshambuliaji huyo ataondoka Etihad Stadium. (Standard)

Klabu ya Leicester City wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter kuhusu kumpa nafasi ya ukocha katika klabu hiyo. (Telegraph)

Bayern Munich wamefufua tena mazungunzo na Fulham kuhusu kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 28. (Sport)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele

Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Ufaransa Tanguy Ndombele, 27, anatazamiwa kuondoka katika klabu ya Tottenham kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Foot Mercato)

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal anasema kuwa kocha mwenzake wa Uholanzi Erik ten Hag hafai kufutwa kazi na klabu hiyo ya Ligi ya Premia. (Metro)

Kiungo wa kati wa Everton Mbelgiji Amadou Onana, 22, anahusishwa na kuhamia Arsenal na anasema angependa kuchezea "klabu ya kimataifa ya dunia". (Standard)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 9 Juni, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 9 Juni, 2024 Reviewed by Zero Degree on 6/09/2024 08:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.