Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 10 Juni, 2024

Armando Broja, 22

Everton wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Albania Armando Broja, 22, kutoka klabu ya Chelsea kwa mkataba wa pauni milioni 30. (Ben Jacobs)

Wolves wamekubali mkataba wa kumsajili mchezaji wa Ureno Rodrigo Gomes, 20 kutoka klabu ya Braga. (Athletic)

Klabu ya Al-Nassr ya ligi kuu ya Saudia iko kwenye mazungumzo ya kumsajili kipa wa Poland Wojciech Szczesny, mwenye umri wa miaka 34, kutoka Juventus. (Fabrizio Romano)

Newcastle wanataka kusajili mshambuliaji mwingine msimu huu wa joto. (Football Insider)

Kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona Xavi angependa kuwa mkufunzi wa klabu ya ligi kuu ya Uingereza. (Sport)

Mmiliki mwenza wa Wrexham Rob McElhenney hajakata tamaa ya mshambuliaji wa zamani wa Wales na Real Madrid Gareth Bale, 34, kusajiliwa na klabu hiyo ya League One.

Arsenal wameambiwa watalazimika kutumia pauni milioni 50 kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz mwenye umri wa miaka 26 kutoka Aston Villa. (Mirror)

Phil Foden, 24

Manchester City wanatazamiwa kumfanya kiungo wa kati wa Uingereza Phil Foden, 24, kuwa mchezaji wa Uingereza anayelipwa zaidi katika historia kwa kupandisha mshahara wake hadi £375,000 kwa wiki. (Sun)

Klabu ya Arsenal na Manchester United bado wanavutiwa na mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 23, ambaye pia anasakwa na AC Milan. (Sky Sports)

Bayern Munich wamewasilisha ofa ya mwanzo ya thamani ya takriban Euro milioni 30 kumnunua kiungo wa kati wa Fulham Mreno Joao Palhinha, 28. (Mail)

Mlinda mlango wa zamani wa Arsenal Jens Lehmann anasema hana uhakika kama kocha wa sasa Mikel Arteta ndiye mtu sahihi kuinoa klabu hiyo. (Telegraph)

Klabu hiyo ya Wales pia iko kwenye harakati za mazungumzo na mlinda mlango wa Uingereza Arthur Okonkwo, mwenye umri wa miaka 22, kuhusu mkataba wa kudumu baada ya kuachiwa na Arsenal. (Talksport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 10 Juni, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 10 Juni, 2024 Reviewed by Zero Degree on 6/10/2024 09:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.