NBCPL2024/23: Dabi ya Kariakoo kuanzia Uwanja wa KMC
Siku moja tu baada ya kumalizika kwa mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga, Bodi ya Ligi, imetoa ratiba ya ligi msimu wa 2024/2025, ikionesha timu hizo zitakutana tena Oktoba 19 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na bodi hiyo, mchezo huo utakuwa wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu, umepangwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam, Simba ikiwa ni mwenyeji.
Hiyo itakuwa fursa nzuri kwa Simba kulipiza kisasi kwani imepoteza mechi zake tatu mfululizo za hivi karibuni dhidi ya watani zao hao, msimu uliopita ilifungwa michezo yote miwili ya Ligi Kuu.
Ilianza kwa kuchapwa mabao 5-1 katika mzunguko wa kwanza mechi iliyochezwa Novemba 5, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, na mchezo wa mzunguko wa pili ikafungwa mabao 2-1, uwanja huo huo, Aprili 20, kabla ya Alhamisi iliyopita kudunguliwa bao 1-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii.

Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi, Simba itafungua dimba la Ligi Kuu, Jumapili ijayo, Agosti 18, dhidi ya Tabora United, mechi ikipigwa Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam, huku Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wakisubiri hadi Agosti 29, watakapoanza ligi kwa kucheza na Kagera Sugar.
Yanga haitocheza mechi ya ligi wiki ya kwanza inayotarajiwa kuanza Ijumaa ijayo kutokana na kuwa kwenye majukumu ya kimataifa, ikitarajiwa kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Vital'0 ya Burundi, Agosti 17.
Timu zingine ambazo hazitocheza mechi yoyote ya ufunguzi wa ligi wiki ijayo ni Azam ambayo itacheza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR na itarejea kucheza Ligi Agosti 28 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Meja Jenerali, Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam huku Coastal Union inayocheza Kombe la Shirikisho Afrika yenyewe itacheza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Agosti 29 dhidi ya KMC, Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

Simba itacheza mechi yake wiki ijayo kwa sababu haipo kwenye hatua ya awali ya mashindano ya kimataifa, itaanzia hatua ya kwanza inayotarajiwa kuanza Septemba.
Ligi Kuu Tanzania Bara itaanza ijumaa ijayo kwa mechi kati ya Pamba Jiji dhidi ya Prisons, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Jumamosi ijayo ligi itaendelea kwa michezo miwili kati ya Mashujaa FC dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, huku Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi, kutakuwa na mechi nyingine kati ya Namungo dhidi ya Fountain Gate.
Jumapili ijayo, mbali na mechi ya Simba dhidi ya Tabora United, kutakuwa na mechi nyingine kwenye Uwanja wa Sokoine wakati KenGold FC itakapovaana na Singida Big Stars.

Reviewed by Zero Degree
on
8/10/2024 03:48:00 PM
Rating: